Na Anna Nkinda – Paris
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete amesisitiza umuhimu wa watoto wenye umri
wa chini ya miaka mitano kupewa chanjo kwa wakati, chakula chenye
virutubisho na kuwafundisha kinamama jinsi ya kuwatunza kwa kufanya hivyo nchi itakuwa inapanda mbegu nzuri na baada ya miaka michache taifa litakuwa na watoto wenye afya bora.
Mama
Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo
(WAMA) ameyasema hayo jana wakati akiongea na wafanyakazi wa Shirika la
Msalaba Mwekundu la nchini Ufaransa ambalo licha ya kutoa huduma
mbalimbali za dharula pia linatoa huduma za afya kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano.
Mwenyekiti
huyo wa WAMA alisema kuwa ili kupunguza vifo vya watoto wenye umri wa
chini ya miaka mitano Serikali kwa kushirikiana na shirika la GAVI
Alliance kupitia wizara ya Afya na Ustawi wa jamii ilitoa chanjo ya
kuzuia magonjwa ya homa ya vichomi na uti wa mgongo nchini Tanzania.
“Taasisi ya WAMA imekuwa ikitoa vifaa tiba inavyochangiwa na wadau mbalimbali katika
hospitali, vituo vya afya na Zahanati ambazo zimekuwa na upungufu
mkubwa wa vifaa hivyo vikiwemo vitanda vya kujifungulia, vitanda vya
kulalia wagonjwa, mashine za kupumulia watoto wanaozaliwa wakiwa na
matatizo.
Pia kwa kushirikiana na shirika la AMREF International taasisi ya hii imetoa mafunzo kwa manesi ambao wameweza kuwaelimisha watoto wa kike walioko mashuleni jinsi ya kujiepusha na mimba za utotoni”, alisema Mama Kikwete.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Uhusiano na Oparesheni za Kimataifa za
Shirika hilo Antoine Peigney alisema kuwa shirika hilo linafanya kazi za
kukabiliana na majanga katika nchi 30 Duniani na limeajiri wafanyakazi
17000 pia watu 20000 kutoka nchi hizo wanafanya kazi za kujitolea.
Alisema
kuwa Shirika hilo limekuwa likilisaidia Shirika la Msalaba Mwekundu
Tanzania pale lilipoombwa kutoa msaada na kutoa mfano mwaka 2004,
2006 na 2009 lilitoa msaada katika mikoa ya Mtwara na Dar es Salaam na
mwaka 2011 katika mkoa wa Manyara hivyo basi watafurahi zaidi kama
watapata nafasi ya kufanya kazi na taasisi ya WAMA ili waweze kuwasaidia
watanzania.
Mama Kikwete ameambatana na Mumewe Rais Jakaya Mrisho Kikwete nchini Ufaransa kwa ajili ya mwaliko wa ziara ya kiserikali ya siku tatu.
0 comments:
Post a Comment