Vibonde wa
Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars (Zambia)
ambao ni Mabingwa wa Soka bara la Afrika leo wamelazimishwa sare na
Wababe wa Stars Ethiopia kwa kufungana 1-1 katika mchezo wao wa kwanza wa
kuwania ubingwa wa Afrika.
Katika
mchezo huo ambao Ethiopia walicheza wakiwa 10 uwanjani, walifanikiwa kufunga
bao la kusawazisha katika kipindi cha pili.
Ethiopia
ambayo inashiriki michuano hiyo kwa mara ya pili baada ya kipindi cha miaka 30
kupita ilikuwa waandike goli katika dakika 20 za awali baada ya Saladin Seid
kupiga mkwaju wa penati uliopanguliwa na mlinda mlango Kennedy Mweene.
Alikuwa ni Collins
Mbesuma aliyewanyanyua mashabiki wa Zambia uwanjani hapo na popote pale duniani
baada ya kuifungia timu yake goli katika dakika ya 44 kipindi cha kwanza na
baadae Adane Girma aliisawazishia Ethiopia katika kipindi cha pili.
Taifa
Stars ilichezo michezo miwili ya kirafiki dhidi ya Zambia hapa nyumbani
na kushinda 1-0 na baade kucheza na Ethiopia mjini Adis Ababa na
kuchapwa goli 2-1.
Michuano ya Mwaka huu ya AFCON imetawaliwa na sare ya bila kufungana au ya kufungana 2-2 au 1-1 huku Mali pekee wakiibuka na ushindi hafifu wa goli 1-0 dhidi ya Niger jana.
0 comments:
Post a Comment