Naibu
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mhe.
Philipo Mulugo ametangaza matokeo ya
Mtihani wa Taifa wa Elimu ya Sekondari Kidato cha Pili mwaka 2012, ambapo kiwango cha ufaulu kimepanda kutoka asilimia
45.40 mwaka 2011 hadi kufikia asilimia 64.55 mwaka 2012.
Matokeo
hayo yametangazwa mbele ya waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam ambapo idadi ya
watahiniwa waliosajiliwa kufanya mtihani walikuwa 430,327, kati yao wasichana
walikuwa 205,476 na wavulana 224,851, ikiwa ni upungufu wa watahiniwa 36,240
ikilinganishwa na mwaka 2011 ambao walikuwa 466,567.
“Watahiniwa
386,271 sawa na asilimia 89.76 ya waliosajiliwa, walifanya mtihani wakiwemo
wasichana 187,244 na wavulana 199,027, watahiniwa 44,056 sawa na asilimia 10.24
hawakufanya mtihani, kati yao wasichana ni 18,231 na wavulana 25,825” amesema
Mulugo.
Aidha Waziri Mulugo amefafanua kuwa
watahiniwa 136,946 ambao wameshindwa kupata wastani wa ufaulu wa alama 30 na
wale waliofutiwa matokeo yao kutokana na udanganyifu watalazimika kukariri
kidato cha pili mwaka 2013.
“Ni vema ikaeleweka kuwa kukariri
kidato si adhabu bali ni kutoa fursa nyingine kwa mwanafunzi kuweza kupata
maarifa, stadi na ujuzi wa elimu ya sekondari, hivyo ni matumaini yangu kuwa
wanafunzi hawa watafanya bidii katika kujifunza na kuzingatia masomo ili waweze
kufaulu masomo yao katika kiwango kinachotakiwa” amesisitiza Mulugo.
Mtihani
wa Taifa wa Elimu ya Sekondari Kidato cha Pili ulifanyika nchini kote kuanzia
tarehe 05 Novemba, 2012 na kumalizika tarehe 16 Novemba, 2012 kukiwa na jumla
ya vituo 4,304 vilivyosajili watahiniwa, sawa na ongezeko la vituo 117
ikilinganishwa na ile ya mwaka 2011.
good,lakini hujatwambia tunaweza kuyapata website gani hayo matokeo!!!!
ReplyDeleteJe majina yameshatoka? na kama yametoka tunaomba mtuwekee.
ReplyDelete