Mwenyekiti
wa Asasi ya Siasa,Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo kusini Mwa
Afika SADC Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (wa pili kulia) akiwa pamoja
na Rais wa Madagascar Andry Rajoelina (kulia),Rais Wa Namibia
Hifikepunye Pohamba (kushoto) na Rais wa Msumbiji Armando
Guebuza, wakati wa kikao cha Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama cha
SADC, kilichofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
******
NA MAGRETH KINABO – MAELEZO
WAKUU wa nchi na Serikali wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuia ya Maendeleo ya Kusini Mwa Afrika(SADC TROIKA) wamekubaliana kusaidiana na umoja wa Mataifa(UN) wa kupeleka Majeshi ya Ulinzi na Usalama(NIF) katika upande wa Mashariki mwa Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo(DRC) .
Kauli hiyo imetolewa leo na Katibu Mtendaji wa Jumuia ya Maendeleo ya Nchi za Kusini Mwa Afrika(SADC), Tomaz Salomao
wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mkutano wa wakuu hao
uliofanyika kwa muda wa siku mbili jijini Dares Salaam.
Mkutano huo ulimalizika leo ambao ulikuwa unajadili hali ya siasa na usalama kwa nchi za DRC, Zimbambwe na Madagascar chini ya Mwenyekiti wake (SADC TROIKA) Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete na kuhudhuriwa na Rais wa Namibia, Hifikepunye Pohamba, Rais wa Msumbiji , Armando Emilio Guebuza, ambaye ni Mwenyekiti wa SADC na Rais wa Msumbiji , Jacob Zuma .
Akizungumzia kuhusu upande wa DRC Salomao alisema “mkutano huo umetaka misaada ya kibinadamu ipelekwe mapema iwezekanavyo katika upande wa Mashariki mwa DRC.
Salomao
aliongeza kuwa wamepokea ahadi za nchi za Malawi, Namibia, Afrika
Kusini na Tanzania za kuwa tayari kupeleka majeshi ya ulinzi na usalama
katika upande huo , ambapo pia umezishauri nchi nyingine ambazo hazijatoa ahadi hizo kufanya hivyo haraka iwezekanavyo.
Akijibu swali la mwandishi wa habari kuwa kila nchi itachangia wanajeshi wangapi na lini watakwenda Rais Kikwete alisema suala hilo bado liko kwenye mchakato.
Kwa upande wa Zimbabwe Salomao alisema mkutano huo umependekeza wadau wa siasa katika nchi hiyo kuhakikisha wanaharakisha wanakamilisha utengenezaji wa Katiba mpya ili kuwezesha uchaguzi wa amani, huru, na haki .
Aliongeza kuwa katika mgogoro wa kikatiba wa nchi ya Madagascar mkutano huo umepokea maelezo, kutoka kwa Rais wa mpito wa nchi hiyo ,Andry Rajoelina kuhusu mkakati wa kutatua suala hilo na kusisitiza utekelezaji wake.
0 comments:
Post a Comment