Nafasi Ya Matangazo

December 03, 2012

Rais Jakaya Kikwete akimkabidhi tuzo Mke wake Mama Salma Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA kwa kutambua mchango wa taasisi hiyo katika mapambano ya Ukimwi wakati wa maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani ambayo kitaifa iliadhimishwa mkoani Lindi kwenye uwanja wa Ilulu na kushirikisha wadau mbalimbali wanaopambana na janga la ugonjwa wa ukimwi, kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Lindi Ludovick Mwananzila
Rais jakaya Kikwete akimkabidhi tuzo Meneja wa PSI Mtwara na Lindi kwa kutambua mchango wa taasisi hiyo katika mapambano ya ukimwi wakati wa maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani yaliyofanyika jana mjini Lindi, kushoto ni Mkurugenzi wa Tume ya kudhibiti Ukimwi TACAIDS Dr. Fatma Mrisho.
Mwenyekiti wa taasisi ya WAMA mama Salma Kikwete akifurahia tuzo hiyo pamoja na wafanyakazi wa taasisi yake mara baada ya kukabidhiwa na Rais Jakaya Kikwete jana katika maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani yaliyofanyika mjini Lindi
Wafanyakazi wa PSI wakionyesha tuzo yao mara baada ya kukabidhiwa kwenye maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani yaliyofanyika mjini Lindi jana.
Baadhi ya wafanyakazi na wadau mbalimbali walioshiriki katika maonyesho hayo kutoka WAMA.SOURCE: FULLSHANGWEBLOGCOM.
Posted by MROKI On Monday, December 03, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo