- Kocha Afurahishwa na Mwinyi Kazimoto kurejea uwanjani
Wakati timu ya Tanzania bara,
Kilimanjaro Stars, ikishuka dimbani leo dhidi ya Rwanda katika michuano ya
Tusker Cecafa Challenge Cup inayoendelea Jijini Kampala, kocha wa timu hiyo, Kim Poulsen
amesema wanaiheshimu Rwanda lakini watakufa nayo katika hatua hii ya robo
fainali.
Aliyasema hayo jana baada ya
mazoezi kika uwanja wa Chuo Kikuu cha Kyambogo ili kujiandaa na mechi hii ya
robo fainali.
“Rwanda ina timu nzuri na
tunaiheshimu sana lakini tuko tayari kupambana nao katika mechi ya kesho na
ninaamini vijana wataendelea kufunga mabao kama ilivyofanyika katika mechi
dhidi ya Somalia,” alisema.
Kocha huyo alisema wachezaji
wote wako katika hali nzuri na wana ari ya kushinda mechi hii ili watinge
katika hatua ya nusu fainali.
Alisema amefurahishwa kuona
mchezaji Mwinyi Kazimoto akirejea uwanjani jeruhiwa wakati wa mechi na Burundi
Jumatano iliyopita “Kwa sasa yuko katika hali nzuri na atacheza mechi ya kesho.
“Vijana wana morali na
wamejiandaa vizuri na mechi hii ya kesho na tuna imani watatupa raha tena kama
Jumamosi.
Katika hatua nyingine, Meneja
wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager George Kaishe ambaye Bia ya kampuni yake
inaidhamini Kilimanjaro Stars, alitoa pongezi kwa Stars kwa kutinga hatua
ya robo fainali.
“Tumekuwa tukifuatilia
mashindano haya kwa njia ya runinga na kwa kweli yameleta hamasa kubwa sana
hasa mchezo wa Jumamosi tulipoifunga Somaliake kwa vya 7-0,” alisema katika
taarifa yake kwa vyombo vya habari.
Bw Kavishe alisema Stars ina
uwezo mkubwa wa kutinga fainali na kurejea nyumbani na kombe hili la Cecafa.
“Watanzania wote lazima wawe
na imani na waiombee dua njema timu yetu ili ishinde…sisi tukiwa wadhamini
tutaendelea kuipa nguvu timu wao watuletee kombe tu,” alisema.
Timu nyingine zinazoshuka
dimbani leo katika Uwanja wa KCC Lugogo Jijini Kampala ni Zanzibar Heroes na
Burundi mechi ambayo itachezwa saa kumi alasiri baada ya ile ya Stars na
Rwanda.
Mechi za Jumanne ni Kenya
dhidi ya Malawi saa Kumi alasiri na baadaye mwenyeji Uganda atashuka dimbani na
Ethiopia katika Uwanja wa Mandela eneo la Nambole.
Fainali za mashindano haya
zitapigwa JUmamosi ijayo Disemba 8 katika uwanja wa Mandela.
0 comments:
Post a Comment