TAARIFA KWA UMMA
Wizara ya Nishati na Madini (MEM) inapenda kuutangazia umma kuwa Serikali inatarajia
kuzindua mradi wa ujenzi wa miundombinu ya kusafisha na kusafirisha gesi asilia
kutoka Mnazi Bay Mtwara na Songo Songo Kilwa hadi Dar es Salaam.
Hafla ya kuweka Jiwe la Msingi wa mradi huo itafanyika tarehe 8/11/2012 Kinyerezi, Manispaa ya Ilala, katika
eneo ambapo mitambo ya kuendeshea mfumo mzima wa gesi itajengwa. Mgeni rasmi katika sherehe hiyo atakuwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
Wananchi wote wa Dar es Salaam na maeneo
yanayozunguka eneo la Kinyerezi mnaalikwa na mnaombwa kufika kwenye eneo la
mradi saa 2.00 asubuhi.
GESI ASILIA KWA MAENDELEO YA TAIFA
Imetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini
0 comments:
Post a Comment