Katibu
wa Mufti wa Zanzibar Sheikh Fadhil Soraga akitolewa katika Chumba cha
Huduma ya Mwanzo katika Hospitali ya Mnazi Mmoja baada ya kurushiwa
Tindi kali na watu wasiojulikana wakati akifanya mazowezi huko katika
Kiwanja cha Mwanakwerekwe.
Katibu
wa Mufti wa Zanzibar Sheikh Fadhil Soraga akipandishwa kwenye Gari ya
Wagonjwa kwa lengo la kuwahishwa katika Hospitali ya Muhimbili Dare es
Salaam baada ya kurushiwa Tindi kali na watu wasiojulikana wakati
akifanya mazowezi huko katika Kiwanja cha Mwanakwerekwe.PICHA NA YUSSUF
SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR.
*********
Na Ali Issa na Mwanaisha Mohamed
Maelezo Zanzibar
Naibu
Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Mahmoud Mussa Wadi amesema kitendo cha
kumwagiwa Tindikali Katibu wa Mufti Mkuu Sheikh Fadhili Soraga si
kitendo cha kiungwana na hakiendani kabisa na utamaduni na mila ya
dini ya kiislamu .
Hayo
ameyasema leo huko Ofisini kwake Mazizini nje kidogo ya Mji wa Zanzibar
wakati alipokutana na waandishi wa habari kufuatia tukio la kujerihiwa
vibaya katibu huyo kwa kumwagiwa tindikali na watu wasio julikana
katika maeneo ya Kwerekwe kwenye kiwanja cha mpira alipokuwa akirudi
mazoezi alfajiri ya leo.
Amesema
kitendo hicho sio cha kiungwana na hakiendani na maadili ya uislamu
kwani dini ya kiislamu siku zote ina amrisha kutenda mema na kukatazana
Mabaya . “Uislamu
ni Dini ya amani, upendo na kuaminiana na hawi mmoja wenu muumini wa
kweli mpaka ampendelee mwezake mema”alisema Naibu Mufti .
Aidha
alifahamisha kuwa waliofanya kitendo hicho wafahamu kuwa wamefanya jambo
baya na kama wanahisi kuwa Sheikh Soraya amefanya kosa wajibu wao ni
kumwita na kumuelekeza kama dini ya kiislamu inavyosisitiza.
Amesema
bila shaka hizo ni chuki binafsi na sio masuala ya uislamu na si vizuri
kumuhusisha mtu na jambo lolote bila ya kufanya uchunguzi kwani
unaweza kumfikiria mtu jambo ambalo halimusu .
Alieleza
kuwa kujeruhiwa kwa Sheikh Soraga ni mbinu za makusudi zilizoandaliwa
na watu kwani awali aliwahi kufuatwa na maadui zake akitokea Mazizini
kuelekea Malindi lakini walipofika Hailesalases dereva wake alibaini
kuna gari inawafuata na aliamua kubadili njia na kupita Bustani ya
Jamuhuri na maadui hawo wakatoweka.
Hata hivyo Naibu Mufti alisema dereva huyo hakuweza kuitambua gari ambayo ilikuwa ikiwafuata. Sheikh
Soraya ameathirika sehemu ya usoni, kifuani na tumboni na hali yake ina
endelea vizuri na amepelekwa Dar es Salamu katika Hospitali ya rufaa ya
Muhimbili kwa matibabu .
0 comments:
Post a Comment