Mkurugenzi
wa Shirika la kazi nchini Tanzania (ILO) Bw. Alexio Musindo akitoa
hotuba yake siku ya kufunga maonyesho ya wajasiria mali MOWE 2012
yaliyokuwa yakifanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es
Salaam.
Balozi wa Malawi nchini Tanzania Bi. Flossie Gomile Chidyaonga akitoa hotuba yake kwa wajasiria mali wa MOWE 2012.
Msichana
Mjasiriamali akipokea cheti cha ushiriki wa MOWE 2012 toka kwa Balozi
wa Malawi Bi. Flossie Gomile Chidyaonga (kushoto). Katikati ni Mwenyekiti wa Taasisi ya MOWE Bi. Elihaika Mrema.
Mkurugenzi
wa ILO nchini Bw. Alexio Musindo (kulia) na Bi. Teddy Rucho wakipokea
cheti cha ushiriki toka kwa balozi wa Malawi katika sherehe za ufungaji
wa maonyesho ya wajasiriamali MOWE 2012.
Balozi
wa Malawi Tanzania Bi. Flossie Gomile Chidyaonga (kushoto), Mkurugenzi
wa ILO nchini Bw. Alexio Musindo sambamba na Mwenyekiti wa MOWE Bi.
Elihaika Mrema (katikati) wakiangalia bidhaa zitokanazo na Mti wa Mbuyu
wakati wa sherehe za ufungaji wa maonyesho ya Wanawake Wajasiriamali
MOWE 2012 yaliyomalizika hivi karibuni katika viwanja vya Mnazi Mmoja
jijini Dar.
Balozi akitembea banda la ILO katika maonyesho ya MOWE 2012.
Balozi wa Malawi akipata maelezo toka kwa team ya ILO walioandaa maonyesho ya MOWE kwa kushirikiana na Taasisi ya WAMA.
Balozi
wa Malawi na Mkurugenzi wa ILO nchini wakinunua mifuko maalumu ya
kuhifazia Laptops na iPad iliyotengenezwa kwa ubunifu mkubwa kwa
kutumia malighafi ya Tanzania Kitenge toka kwa Mwanamke Mjasiria mali wa
MOWE 2012 katika maonyesho hayo.
Bwana Pius Mikongoti wa GS1 akitoa Mada kuhusu Barcode kwa washiriki wa MOWE 2012.
Picha ya Pamoja Kamati ya MOWE na wageni rasmi siku ya kufunga maenyesho ya MOWE 2012.
0 comments:
Post a Comment