Meneja
Mradi wa shirika lisilo la kiserikali kutoka Ujerumani ( EIFL) Monica ELBERT
(mzungu) akiwaangalia baadhi ya wanafunzi
wa shule ya msingi Chang’ombe
Mazoezi wilaya ya Temeke mkoani Dar- es- Salaam wakifanya mafunzo pamoja jinsi
ya kutumia teknolojia ya upashanaji wa habari na mawasiilano kupitia mtandao , Mradi huo wa mafunzo ujulikanao
(Public Library Innovation Programme- PIP- ) Kwa kupitia mradi huo wanafunzi wataweza
kupata taarifa mbalimbali kirahisi kwaajili ya masomo yao na taarifa mbalimbali za kila
siku.. Meneja wa mradi huo amefurafahishwa sana baada ya kuhojiana na
wanafunzi hao na kumueleza kwamba ni ukombozi kwao kwani baada ya kumaliza mafunzo, elimu itakuwa imewasaidia sana kuwarahisishia
masuala mbalimbali ya masomo pamoja kupata taarifa mbalimbali, (Picha na
Mwanakombo Jumaa- MAELEZO).
wanafunzi wakifurahia matumizi ya mtandao
0 comments:
Post a Comment