kundi kubwa la ng'ombe katika poli la hifadhi ya
selous
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Said
thabity Mwambungu, wakati akiongea na Viongozi wa Serikali Wilayani Tunduru
kutokana ukiukwaji wa taratibu za kuingiza wanyama hao bila kufuata taratibu
hali ambayo inaweza kuleta madhala na kuzuka kwa mapigano makubwa baina ya
wakulima na wafugaji.
Bw. Mwambungu akatumia nafasi hiyo kumtaka Mkuu wa
Wilaya hiyo Bw. Chander Nalicho na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo
Bw.Albert Nehata kusimamia zoezi hilo na kuhakikisha kuwa Watendaji wa Vijiji,
Wenyeviti wa Vitongoji, Maafisa tarafa kuhakikisha kuwa wanasimamia kwa nguvu
zao zote utekelezaji wa tukio hilo na kwa kiongozi anaye jiona kuwa hata mudu
basi aachie dhamana hiyo aliyopewa na Serikali.
Wakiongea kwa nyakati tofauti baadhi ya madiwani wa
halmashauri ya Wilaya ya Tunduru ililidhia kupokea Ng’ombe elfu kumi tu (10,000)
na wafuagaji hao kutengewa maeneo katika kata za Mhuwesi, Masonya na Ngapa
lakini cha kushangaza wafugaji hao wamekuwa wakiongezeka siku hadi siku na
kuenea katika maeneo yote ya Wilaya hiyo.
Wanachi wa wilaya ya Tunduru wamelalamika kuona
wafugaji hao kuendelea kuvamia hadi katika hifadhi ya Taifa ya Selous, na
hifadhi zamapori tengefu amabazo hutumika katika bishara ya uwindishaji wa
Kitaali zilizopo katika maeneo mbali mbali ya vijiji vilivyo Wilayani humo huku
kukiwa na makatazo ya kuwazuwia wanachi kuingia na hata
kulima.
Afisa Kilimo na Migfugo wa Wilaya ya Tunduru Bw. Chiza
Malando mbali na kukiri kwa uingizaji holela wa mofugo hiyo alisema kuwa hivi
sasa Wilaya ya Tunduru imeonekana kuelemewa na wingi wa mifugo hiyo,kwani hadi
sasa Wilaya hiyo inakadiliwa kuwa na zaidi ya Ng’ombe 40,000 kutoka kwa wafugaji
hao tofauti na malengo ya kuwa na Ng,ombe 10,000
0 comments:
Post a Comment