Emmanuel Okwi
Timu ya Soka ya Simba yenye maskani yake
mtaa wa Msimbazi jijini Dar es Salaam leo
imezidi kujichimbia kileleni baada ya kubugiza bila huruma timu ya Azam magoli
3-1, katika mchezo wa Ligi kuu Soka Tanzania bara uliopigwa kwenye uwanja wa
Taifa.
Mchezaji Emmanuel Okwi wa Simba leo
ameng’ara katika mchezo dhidi ya Azam baada ya kuifungia timu yake magoli 2
huku Mzambia Felix Sunzu akipachika goli la kusawazisha.
Mbali na kichapo hicho Azam ambayo kama
Simba ilikuwa inashikilia rekodi ya kutopoteza mchezo hata mmoja tangu ligi
ianze, lakini leo imevunjiwa mwiko wake huo na kupoteza mchezo na kushuka
nafasi moja kutoka yapili hadi ya tatu.
Yanga iliyokuwa inakipiga na JKT Oljoro
mjini Arusha imepanda kwa mara ya kwanza hadi nafasi ya pili tangu ligi hii
ianze baada ya kufikisha pointi 20, huku watani wao wa jadi Simba wakiwa mbele
kwa Point 2 na Azam ikibaki na pointi 19.
Simba ndio imekuwa timu pekee hadi sasa
mabayo haijapoteza mchezo hata mmoja huku ikiwa imetoka sare mara 4 na kushinda
michezo 6.
0 comments:
Post a Comment