Askari
wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), wakiwa katika Maeneo ya
Kariakoo na viunga vyake kuhakikisha usalama wa raia na mali zao
unaimarika .
Muumini
wa dini ya Kiislamu akishahadia kwa mola wake na kusema nipo tayari
kufa kwa ajili ya kutetea dini ya Allah baada kukamatwa na Askari wa
Kikosi cha Kutulia Ghasia katika viunga vya eneo la Ikulu. (Picha zote na Happiness Mnale)
Safari ya kuelekea Kituo Kikuu ilianza
Askari
wa Kikosi cha kutuliza Ghasia (FFU) wakimwingiza katika gari muumini wa
Kiislamu aliyekamatwa katika viunga vya maeneo ya Ikulu
Barabara
ya kuingia katika Ofisi za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi zikiwa
zimefungwa na Askari Polisi kufuatia vurugu zilizotokea leo
Polisi wakifanya doria kwa kutumia pikipiki
Mitaa
ya Kariakoo na viunga vyake ikiwa imeimarishwa na Askari wa Jeshi la
Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika mitaa ya Kariakoo leo
Ulinzi uliimarishwa na Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania katika mitaa ya Kariakoo leo
Wanajeshi wakivinjari katika mitaa ya Kariakoo leo
Askari
wa jiji wakishiriki kikamilifu katika zoezi la kuwakamata watu
waliokuwa wamekusanyika kwa nia ya kutaka kuandamana katika eneo la
Kariakoo
Magari
ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania wakiwa katika doria katika barabara ya
Msimbazi ambako kulitokea vurugu zilizosababishwa na waislamu waliotaka
kuandamana.
Watu
hao walifika mmoja mmoja maeneo ya Ikulu kabla ya kudhibitiwa na Askari
wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) na kupelekwa Kituo Kikuu cha Kati. Kukamatwa
kwa watu hao kunafuatia Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam
kuwatawanya waumini wa dini ya Kiislamu ambao walikuwa na nia ya kufanya
maandamano.
Waandishi wameshuhudia gari mbili za jeshi la Polisi zikiwa zimebeba wanajeshi waliokuwa na silaha. Katika maeneo ya Kariakoo vikosi vya Jeshi la wananchi wa Tanzania vimekuwa vikifanya doria ili kuimarisha hali ya ulinzi.Picha kwa hisani ya Happiness Mnale
Hawa waislamu hawajui wafanyalo wengine wanafuata mkumbo wanajua labda kuna wali wanajidanganya kabisa kuvuruga amani ya Tanzania. Mi wameniuzi yaanioa kichizi labda siyo watanzania ni wasomalia maana sisi hatuko hivi.
ReplyDelete