Mdhamini Mkuu wa Ligi kuu ya
Vodacom Tanzania bara, kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania, imewekeza
katika kuwawezesha mashabiki wa soka kupata taarifa na matukio ya mechi zote za
ligi hiyo kupitia njia ya simu za kiganjani na intanet.
Kupitia mifumo mbalimbali ya
kiteknolojia wateja wa Vodacom wataweza kupata matokeo ya mechi mbalimbali
kupitia simu zao za kiganjani ukiwa na ujumbe mfupi wa maneno na mitandao ya
kijamii.
Akizungumzia hatua hiyo Mkurugenzi
Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Rene Meza, amesema, Mtandao wa Vodacom una
miundombinu ya kutosha na unaongoza katika masuala ya teknolojia. Hivyo
itatumika katika kuwawezesha mashabiki wa soka walioko ndani na nje ya
nchi kujua matukio mbalimbali ya ligi kuu ya Vodacom.
“Licha ya ligi yetu kuonekana katika kituo
cha Televisheni cha Super Sport. Tumejipanga sasa kuhakikisha inakuwa katika
mitandao mbalimbali muda wote kwa kila mchezo na kila tukio katika soka,
Mashabiki watapata taarifa za ligi popote watakapokuwa,” alisema Meza na
Kuongeza kuwa, “Kupitia intanet matukio haya yatapatikana kupitia
Facebook na Twitter na mitandao mingine ya kijamii.”
“Ili kupata matokeo na taarifa
mbalimbali kupitia njia ya simu mteja wa Vodacom atatakiwa kupiga *149*01# kisha
atachagua VODACOM FLAVA na akisha kujiunga na huduma hiyo itakayo
muwezesha kupata taarifa na matokeo ya mechi mbalimbali”
Aliongeza kuwa, “ Kwa wateja wanaotumia
facebook na twitter kwao ni rahisi zaidi kwani huduma hizo zinatolewa bure na
Vodacom, hivyo mashabiki wa soka watatembelea Ukurasa wetu wa facebook na
Twitter na kupata taarifa mbalimbali kuhusu ligi na wengine kujishindia zawadi
kwa kujibu maswali mbalimbali zikiwemo tiketi za mechi za ligi,”
Aidha Mkurugenzi huyo alitoa Pongezi kwa
Vyombo vya habari kwa kazi kubwa inayofanya katika kuwahabarisha watanzania
kuhusu michezo mbalimbali hususani ligi kuu ya Vodacom kupitia Televisheni,
Radio, Magazeti na Mitandao ya kijamii.
“Vyombo vya habari ni wadau wakubwa na
wanafanya kazi nzuri sana katika kutoa taarifa hizi wanastahili pongezi, nasi
tunaangalia namna ya kuwaunga mkono kwa namna moja ama nyingine katika jitihada
za kukuza soka la Tanzania na tunaamini tutafika mbali.”
Mkurugenzi huyo alihitimisha kwa kutoa
pongezi kwa timu mbalimbali zinazoshiriki katika ligi kwa kusema kuwa
zimeonesha hamasa kubwa na kubainisha kuwa ni ishara ya ukuaji wa soka katika
soka la Tanzania ambalo ndio lengo kuu la Vodacom.
“Ligi sasa imekuwa na msisimko kila timu
inajitahidi kushinda kila mech,hadi sasa timu zote zimeonesha kiwango kikubwa
na soka la kuvutia tunatarajia maendeleo haya yataleta tija hata kwa timu yetu
ya Taifa kufanya vizuri. Vipaji vingi vinaonekana na ajira kwa vijana
imeongezeka kupitia michezo,” alihitimisha Meza.
Kampuni ya Vodacom katika kuongeza
msisimko kwa mashabiki wa ligi imetoa ofa mbalimbali msimu huu kwa kuwawezesha
wateja wake kupata SMS 50, Muda wa maongezi wa dakika 30 na MB 50 kwa shilingi
400 Ili kuwasiliana na ndugu jamaa na marafiki.
Pamoja na mambo mengine kampuni hiyo
inaangalia namna ya kutoa adha ya ukataji tiketi kwa wateja wake kutumia huduma
ya M - pesa kununua tiketi za mechi mbalimbali.
0 comments:
Post a Comment