Nafasi Ya Matangazo

October 18, 2012

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge inayoshughulikia mambo ya Maendeleo ya Jamii wakiwa katika ziara ya kutembelea eneo la Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Kigambini unaosimamiwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),uliopo eneo la Kurasini Jijini Dar es Salaam leo.
Meneja Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Kigamboni kutoka Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Karim Mattaka (kushoto) akifafanua jambo kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge inayoshughulikia mambo ya Maendeleo ya Jamii chini ya Mwenyekiti wake,Mh. Jenista Mhagama (wa pili kushoto) wakati Kamati hiyo ilipofanya ziara ya Kutembelea Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Kigamboni unaosimamiwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) uliopo katika eneo la Kurasini jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mjumbe wa Kamati hiyo na Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki,Mh. Joshua Nassari na wa pili kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Dkt. Ramadhan Dau.
Meneja Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Kigamboni kutoka Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Karim Mattaka (katikati) akionyesha sehemu ya ujenzi wa Daraja hilo unaoendelea hivi sasa katika eneo la Kurasini mpaka Kigamboni wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge inayoshughulikia Maendeleo ya Jamii ilipofanya ziara ya kuona ujenzi wa Daraja hilo leo.Watano Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo,Mh. Jenista Mhagama na Kulia ni Waziri wa Kazi na Ajira Mh. Gaudencia Kabaka. 
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Dkt. Ramadhan Dau (kulia) akiuongoza ujumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge inayoshughulikia mambo ya Maendeleo ya Jamii,iliyofanya ziara ya kutembelea eneo la ujenzi wa Daraja la Kigamboni mapema leo.Wengine pichani toka kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo,Mh. Jenista Mhagama,Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Gaudencia Kabaka na Mjumbe wa Kamati hiyo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mtera,Mh. Livingston Lusinde.
Kamati ya Kudumu ya Bunge inayoshughulikia mambo ya Maendeleo ya Jamii ikipatiwa maelezo mbali mbali juu ya ujenzi wa Daraja hilo ambalo ujenzi wake utachukua takribani miezi 36 mpaka kukamilika kabisa.Daraja hilo lina urefu wa mita 680 na litakuwa na jumla ya barabara sita ambazo tatu zitakuwa zinakuja mjini na zingine za kuelekea Kigamboni
Posted by MROKI On Thursday, October 18, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo