Afisa
uhusiano na matukio wa Airtel Dangio Kaniki akiwapatia chai watoto
shule ya Uhuru Mchanganyiko wakati Airtel ilipotembelea shule hiyo
itakayofaidika na mpango maalumu wa Airtel kwa kushirikiana na BAMVITA
wenye lengo la kuchangia vitabu kwa watoto wenye mahitaji maalum .
Airtel imeanza kutembelea shule zilizopo Dar es Salaam pamoja na mikoani
na kubainisha matatizo wanayokumbana nayo ili kuona namna ya kuwasaidia
watoto hao wenye mahitaji maalum.
Meneja
huduma za jamii wa Airtel Hawa Batuli (katikati)akiongea na mwalimu
mkuu wa shule ya Uhuru Mchanganyiko Anna Mang'enya wakati Airtel
ilipotembelea shuleni hapo jana. Airtel imeanza kutembelea shule
zilizopo Dar es Salaam pamoja na mikoani na kubainisha matatizo
wanayokumbana nayo ili kuona namna ya kuwasaidia watoto hao wenye
mahitaji maalum. Kushoto ni Afisa uhusiano na matukio wa Airtel
Dangio Kaniki
Afisa
uhusiano na matukio wa Airtel Dangio Kaniki akinywa chai pamoja na
watoto wa shule ya Uhuru Mchanganyiko wakati Airtel ilipotembelea shule
hiyo itakayofaidika na mpango maalumu wa Airtel kwa kushirikiana na
BAMVITA wenye lengo la kuchangia vitabu kwa watoto wenye mahitaji maalum
. Airtel imeanza kutembelea shule zilizopo Dar es Salaam pamoja na
mikoani na kubainisha matatizo wanayokumbana nayo ili kuona namna ya
kuwasaidia watoto hao wenye mahitaji maalum.
Meneja
huduma za jamii wa Airtel Hawa Batuli (kushoto) akimshukurua mwalimu
mkuu wa shule ya Uhuru Mchanganyiko Anna Mang'enya kwa kuwapokea
walipotembelea shule hapo ambapo Airtel imeanza kutembelea shule
zilizopo Dar es Salaam pamoja na mikoani na kubainisha matatizo
wanayokumbana nayo ili kuona namna ya kuwasaidia watoto hao wenye
mahitaji maalum. Kushoto ni Afisa uhusiano na matukio wa Airtel
Dangio Kaniki
======== ======= ========= =========
Kampuni
ya simu za mkononi ya Airtel imewahimiza watanzania kuendelea kuchangia
katika mradi wa kuchangia vifaa kwa ajili ya watoto wenye mahitaji
maalum unaoendeshwa na Kampuni ya Airtel kwa kushirikiana na Baraza la
maendeleo ya vitabu Tanzania (Bamvita).
Afisa
uhusiano na matukio wa Airtel Dangio Kaniki amesema kampuni hiyo ikiwa
na Balozi wake, AY imeanza kutembelea shule zilizopo Dar es Salaam
pamoja na mikoani na kubainisha matatizo wanayokumbana nayo ili kuona
namna ya kuwasaidia watoto hao wenye mahitaji maalum. Airtel inaamini
kwamba watoto hao wenye mahitaji maalum wakiwezeshwa kielimu wataweza
kutimiza ndoto zao na kuchangia katika maendeleo ya kiuchumi nchini.
Akiongea
wakati walipotembelea shuleni hapo Meneja huduma kwa jamii Hawa Bayumi
alisema ” Ni matumaini yetu kuwa watanzania na wale wasio watanzania kwa
ujumla wataendelea kutuunga mkono ili kuweza kutimiza lengo hili la
awali na kisha kuongeza shule za mikoani mara baada ya kukamilisha
mahitaji haya katika shule hizi za Dar es Salaam. Kampeni hii
itaendeshwa kwa muda wa miezi mitatu , na watanzania wanaweza kuchangia
kwa kutuma neno “Vitabu” kwenda namba 15626 na utakuwa umechangia
shilingi 200 katika mradi huu au kupitia Airtel Money
unapiga *150*60# ingiza jina la biashara VITABU na kuchangia kiwango
chochote kile.
Tunachukua fulsa hii kuwaomba watanzania wote kuchangia ili kuwafikia watoto wengi zaidi nchin” Nae
Mwalimu Mkuu wa shule ya Uhuru Mchanganyiko Anna Mang'enya amesema
“shule hiyo inakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo uhaba wa vifaa
vya kufundishia. bila vifaa hivyo maalum itakuwa vigumu kwa wanafunzi
kutimiza ndoto zao zakuendelea kielimu”.
Aidha
Ameishukuru Airtel na BAMVITA kwa kuweza kuanzisha mradi huu na kuweza
kuwahamasisha watanzania kuchangia ili waweze kupata vitendea kazi na
kuongeza kuwa shule hiyo bado inakabiliwa na changamoto nyingi katika
elimu hivyo kuiomba kampuni hiyo kuendelea kuisaidia katika mambo
mengine.
Zena
Yahaya Mwanafunzi Uhuru Mchanganyiko alikuwa na haya ya kuongeza
“tunawashukuru Airtel kwa kuja kututembelea leo, tunawaomba watanzania
wote waendelee kutusaidia kwa kushirikiana na Airtel katika mradi huu
wa Vitabu ili kuweza kutusaidia katika kununua vifaa vya kutusaidia hapa
shuleni na kuhakikisha tunapata elimu bora.”
Airtel
inatambua umuhimu wa Elimu na tunaamini Tanzania itajengwa na sisi
wenyewe hivyo basi lengo la mradi huu ni kutoa nafasi kwa jamii yetu
kuweza kuchangia elimu ya msingi kwa watoto wenye mahitaji maalum kwa
kuwanunulia vitabu na nyenzo za walimu kufundishia. Kwa kuanzia tumeanza
kutembelea shule mbili za jijinini Dar es Salaam zitafaidika na mpango
huu ambazo ni Sinza Maalum, Uhuru Mchanganyiko ikifuatiwa na Buguruni
Viziwi
0 comments:
Post a Comment