Waziri
Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli, Edward Lowasa akisalimiana na Mrembo wa mkoa
wa Rukwa ambaye anaiwakilisha kanda ya Kaskazini, Vency Edward. Warembo
wanaowania taji la Redds Miss Tanzania 2012
walimtembelea nyumbani kwake eneo la Ngarash mjini Monduli, mkoani
Arusha.
Warembo wakiuliza Maswali yao kwa Mheshimiwa Lowasa.
Mbunge wa Monduli nuu Mstaafu, Mh. Edward Lowasa akijibu maswali ya warembo. Kushoto ni Mkewe, Regina Lowasa na Wengine ni Mkurugenzi wa Lino International Agency, Waandaaji wa Miss Tanzania Hasim Lundenga na Miss Tanzania 2011, Salha Izrael.
Na Father Kidevu Blog, Ngarash-Monduli
WAZIRI Mkuu Mstaafu wa Tanzania, na Mbunge wa Monduli, Edward Lowasa amewataka warembo wanaoshiriki mashindano ya urembo ya Redds Miss Tanzania 2012 kutumia nafasi hiyo waliyopata kutengeneza ajira kwao na vijana wenzao.
WAZIRI Mkuu Mstaafu wa Tanzania, na Mbunge wa Monduli, Edward Lowasa amewataka warembo wanaoshiriki mashindano ya urembo ya Redds Miss Tanzania 2012 kutumia nafasi hiyo waliyopata kutengeneza ajira kwao na vijana wenzao.
Lowasa
ameyasema leo wakati warembo wanaowania taji hilo walipomtembelea nyumbani
kwake eneo la Ngarash mjini Monduli na kuzungumza nao juu ya mambo mbalimbali
ya kisiasa, uchumi, utalii na sanaa ya urembo.
“ninyi
ni vijana, mnanguvu na hakika mkiyatumia vyema mashindano haya kwa malemngo
yanayostahili mnaweza kufika mbali kimaisha kwa kuwa wabunifu wa vitu
mbalimbali vya kufanya katika jamii na kujipatia ajira yenu binafsi na hata
kuajiri watu wengine,”alisema Lowasa.
Lowasa
ambaye amekuwa mstari wa mbele nchini katika kuhakiskisha vijana wengi wanapata
ajira nchini amesema sanaa ya urembo ikitumika vyema inamanufaa katika jamii na
ikitumiwa vibaya italeta matatizo na kuonekana sio kitu cha muhimu.
Akitolea
mfano wa Washindi wa Taji la Miss Tanzania waliopita hasa Hoyce Temu ambaye ni
Miss Tanzania 1999 kwa jinsi alivyo kuwa
mbunifu na kipindi chake cha Mimi na Tanzania ambacho mbali na kutoa fursa ya
kuweza kuibua matukio na maisha ya hali tofauti ya Watanzania lakini pia ametoa
ajira kwa wote anaofanya nao kazi.
Akizungumzia
juu ya ziara hiyo ya warembo hao ya kutembelea Vivutio vya Utalii nchini hasa
katuka Mikoa ya Kanda ya Kaskazini amesema kuwa ni jambo jema hasa kuziangatia
kuwa utangazaji wa vivutio vya utalii vya nchi yetu upo chini hivyo warembo
watasaidia jamii kuelewa na kujenga utamaduni wa kuitembelea vivutio vya utalii
na kuhamasisha utalii wa ndani.
Kuhusiana
na hali ya kisiasa nchini Lowasa amewaambia warembo hao kuwa Tanzania ipo
katika hali nzuri ya kisiasa jambo ambalo linazidi kuchochea maendelea na
kuleta umoja wa kitaifa ambao unawawezesha watu kuishi kwa amani.
“Siasa
yetu ni safi na kiukweli Serikali ya CCM inazidi kuidumisha hali ya amani
nchini jambo ambalo linawezesha hata ninyi kutembea bila matatizo kutoka sehemu
moja hadi nyingine, alisema Lowasa.
Pia
Lowasa aliipongeza Kamati ya Miss Tanzania chini ya Mkurugenzi wakew Hashim
Lundenga kwa kazi kubwa ya kuandaa mashindano hayo makubwa nchini ambayo
yamekuwa yalityoa ajira mbalimbali kwa washiriki wake na fursa za elimu.
Warembo wanaowania taji la Redds Miss Tanzania wapo
katika ziara ya kutembelea vivutio vya utalii Kanda ya Kaskazini pamoja na
kufanya shughuli za kijamii ikiwa ni pamoja na kuchangia watoto yatima na
waishio katika mazingira magumu.
Kesho
Oktoba 11, watatembelea Hifanyi ya Bonde la Ngorongoro na kujionea maajabu
mbalimbali yaliyopo katika eneo hilo.
0 comments:
Post a Comment