The
Deputy Minister of State in the Vice-President's Office (Environment),
Charles Kitwanga (3rd left) and the Deputy Minister for Energy and
Minerals, Stephen Masele (right), inaugurate a water well at Nyaisangero
village in Tarime district, Mara region, built by African Barrick
Gold's (ABG) North Mara Mine as part of its vast community investment
projects.
The
Deputy Minister for Energy and Minerals, Stephen Masele (2nd right),
inaugurates the Sungu Sungu hospital in Tarime district, Mara region,
after African Barrick Gold's (ABG) North Mara Mine spent around $330,000
(more than 500 million shillings) to rehabilitate and upgrade the
hospital. Looking on are ABG's Vice President for Corporate Affairs, Deo
Mwanyika (right), Deputy Minister of State in the Vice-President's
Office (Environment), Charles Kitwanga (3rd right) and the General
Manager of North Mara Mine, Gary Chapman.
The
Deputy Minister of State in the Vice-President’s Office (Environment),
Charles Kitwanga, addresses journalists after his recent visit to
African Barrick Gold’s (ABG) North Mara mine.
he
Deputy Minister of State in the Vice-President’s Office (Environment),
Charles Kitwanga, inspects operations of the North Mara gold mine during
his recent visit to the mine owned by African Barrick Gold (ABG).
*********
MWANDISHI WETU,Tarime
SERIKALI
imeipongeza kampuni ya African Barrick Gold (ABG) kwa kuleta manufaa
makubwa kwa taifa kutokana na uwekezaji unaoendelea kufanywa na migodi
yake nchini katika nyanja mbalimbali ikiwemo uchumi wa nchi
na maendeleo ya jamii.
Kampuni
ya ABG inamiliki migodi minne ya dhahabu nchini -- Bulyanhulu, North
Mara, Buzwagi na Tulawaka na ndiyo kampuni kubwa kuliko zote kwenye
sekta ya madini. “Nimejifunza
mambo mengi sana baada ya kutembelea mgodi wa North Mara,” alisema
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Stephen Masele, siku ya Ijumaa baada
ya kufanya ziara ya mgodi huo wa ABG ulioko wilaya ya Tarime, mkoa wa
Mara.
Katika
ziara hiyo, Masele pamoja na Naibu Waziri wa Nchi kwenye Ofisi ya
Makamu wa Rais (Mazingira), Charles Kitwanga, walitembelea miradi
mikubwa ya jamii ambayo inatekelezwa na mgodi huo kwenye sekta
mbalimbali ikiwemo elimu, maji na afya.
Masele
alisema kuwa mgodi wa North Mara kihistoria umekuwa na matatizo ya
mahusiano na jamii inayoizunguka, lakini hatua kubwa zimepigwa sasa
kuboresha mahusiano na vijiji vinavyozunguka mgodi huo. “Mimi
binafsi Bungeni nimeskia pale wabunge wa huku wakilalamika kwamba kuna
shule za msingi ziko jirani sana na mgodi. Kazi za mgodi zinapoendelea,
ile milipuko inakuwa ikiwaathiri wanafunzi,” alisema.
“Lakini
leo nimetembelea shule ambayo inatakiwa kujengwa ili kuhamisha ile
ambayo inaathiriwa na shughuli za mgodi. Nimejionea kazi ambayo
inaendelea pale. Wakandarasi wako saiti wanajenga hizo shule.” Masele
alisema kuwa kipindi cha nyuma kulikuwa na tatizo la wanafunzi kukaa
chini katika shule zilizopo katika maeneo hayo ya mgodi, lakini mgodi wa
North Mara sasa unatekeleza mradi kabambe wa kuzipatia shule hizo
madawati.
“Nimejionea
kwamba mgodi umeweza kutekeleza ahadi ya kuweka madawati katika shule
zote ambazo zinazunguka mgodi na wanafunzi wamekaa kwenye madawati,”
alisema. Hivi
karibuni, mgodi wa North Mara ulitoa msaada wa zaidi ya madawati 1,000
kwa shule za msingi za Wilaya ya Tarime ambazo zinazunguka mgodi huo.
MIRADI YA MAJI
Waziri
Masele pia ameipongeza ABG kwa jitihada zake za kutoa msaada kwa
wananchi kuhakikisha kuwa wanapata huduma ya maji safi na salama ya
kunywa.
“Palikuwa
na wasiwasi mkubwa wa maji … wananchi walikuwa wakilalamika wanachota
maji mbali. Leo nimeshuhudia tukizindua kisima cha maji ambacho ni moja
ya mwendelezo wa visima vya maji vingine na miradi ya
maji mingine ambayo mgodi inaendelea kutekeleza kwa wananchi,” alisema.
“Akina
mama ambao walikuwa wakiamka saa saba au saa nane usiku kwenda kutafuta
maji sasa wanaweza kuamka saa mbili au saa moja asubuhi. Nimeona
bowsers (malori ya maji), maji wanaletewa mlangoni kitu ambacho maeneo
mengi tungependa kuletewa maji mlangoni lakini eneo hili la Nyamongo
sasa wananchi wanapelekewa maji mlangoni na mgodi wa Barrick.”
SEKTA YA AFYA
Mawaziri
hao pia walitembelea hospitali ya Sungusungu ambayo mgodi wa North Mara
ulikabidhi kwa serikali baada ya kutumia zaidi ya dola za Marekani
330,000 (zaidi ya shilingi milioni 500) kufanya ukarabati mkubwa katika
hospitali hiyo.
“Vijana
wengi hapa wanajishughulisha na shughuli za uchimbaji madini na
wanapata ajali nyingi. Tumeshuhudia pale vijana wanapata ajali lakini
wanatibiwa katika hospitali ambayo imejengwa na mgodi ambayo zamani
ilikuwa ni hospitali ndogo sana,” alisema.
Masele
alitaka migodi mingine nchini iige mfano wa mgodi wa North Mara wa ABG
kwenye kuboresha mahusiano na jamii na kuwekeza kwenye miradi mikubwa ya
maendeleo ya jamii.
“Tumeona
shughuli zile za kijamii kama community development projects
zinafanyika kwa ufanisi na kwa kasi kubwa. Hili binafsi mimi
limenifariji kwa sababu yale ambayo tumeyaahidi kwa wananchi kwamba
tutahakikisha tunaisimamia migodi hii ilete manufaa kwenye jamii zote
ambazo zinazoizunguka,” alisema.
KODI ZA MADINI
Masele
aliipongeza ABG kwa kutoa mchango mkubwa kwa pato la taifa kupitia
kwenye kodi mbalimbali ambazo migodi yake inalipa serikalini.
“Kwa
upande wa shughuli za kodi, tunaendelea na mazungumzo na tunaishukuru
Barrick kwa ujumla na migodi yao yote siyo tu North Mara, hata mingine
yote kwa ujumla wameweza kuhama kutoka kwenye kulipa mrabaha wa asilimia
3 na sasa wanalipa asilimia 4 ya mapato yote,” alisema.
“Hii
ni hatua kubwa ambayo wameifanya ambayo iko nje ya mikataba yao ambayo
waliifunga huko nyuma. Sasa unaweza kuona kuwa wametoa ushirikiano
mkubwa kwa serikali kuweza kukubali kulipa asilimia 4 ya mrabaha, jambo
ambalo limeongeza mapato katika makusanyo ya serikali.”
TAARIFA YA KUUZWA KWA ABG
Masele
alikanusha tetesi kuwa tayari kampuni ya ABG imekwishauzwa kwa kampuni
ya taifa ya dhahabu ya China na kusisitiza kuwa serikali inafuatilia kwa
karibu mazungumzo kati ya kampuni hizo.
“Kuna
taarifa nyingi zimesikika kwenye vyombo mbalimbali vya habari kwamba
mgodi utanunuliwa na wengine wameshasema kuwa umeshauzwa. Naomba niseme
tu kuwa mgodi bado haujauzwa lakini mazungumzo ya kuuzwa mgodi na kununuliwa na kampuni ya taifa ya China yanaendelea kati yao,” alisema.
“Sisi
kama serikali la kwetu ni moja tu, maslahi yetu kama nchi kwenye kodi na
maslahi mengine yote. Zipo kodi nyingi sana ambazo serikali inazipata
kutoka kwenye mgodi.”
UWEKEZAJI WA ABG
Makamu
wa Rais wa ABG wa shughuli za shirika, Deo Mwanyika, alisema kuwa mgodi
wa North Mara umeingia mkataba na vijiji vyote vinavyouzunguka wa
kuwekeza zaidi ya dola za Marekani milioni 8.5 (zaidi ya shilingi
bilioni 13) kwenye miradi mbalimbali ya jamii ikiwemo kwenye sekta za
elimu, afya na maji.
Mwanyika
alisema kuwa mgodi wa North Mara unakabiliwa na changamoto mbalimbali,
ikiwemo tatizo la uvamizi wa mara kwa mara unaofanywa na baadhi ya
wananchi kwenye eneo la mgodi huo.
“Changamoto
kubwa sana ya mgodi huu pamoja na uzalishaji ni mahusiano na jamii.
Kulikuwa na malamiko makubwa sana kuhusu kutotekeleza mikataba ambao
mgodi ulikuwa umeingia huko siku za nyuma. Sisi tumetoa ahadi kuwa
tutatekeleza hiyo mikataba yote na tumeanza,” alisema.
“Changamoto
zipo, bado tuna tatizo kubwa la uvamizi lakini kwa kiasi kikubwa
tunafanya kazi na serikali na ujio wa hawa mawaziri wawili mojawapo ni
kuangalia kwa kiasi gani tunaweza kukaa kwa pamoja tukapunguza haya
mambo ya uvamizi bila kuleta madhara kwa wananchi.”
0 comments:
Post a Comment