Nafasi Ya Matangazo

September 07, 2012


Mkurugenzi Mkuu wa  Tume Ya Usuluhishi na Uamuzi (CME) kutoka Wizara ya Kazi na Ajira Cosmas Msigwa, akisoma chapisho lenye maelezo  ya Kanuni mbalimbali za ajira na mahusiano kazini, jijini Dar es Salaam mbele ya waandishi wa habari ( hawapo pichani,) wakati wa semina ya siku moja kwa wanahabari kuhusu taratibu za kutatua migigoro ya kila siku na changamoto zake sehemu za kazi Tanzania  ambapo wanahabari kupitia vyombo vyao waweze kusaidia kutoa elimu hii kwa  waajiri na waajiriwa pamoja na jamii nzima ya watanzania kwa ujumla kupitia vyombo vyao. Semina hiyo ilifanyika leo Septemba 7, 2012 Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa  Tume ya Usuluhishi na Maamuzi (CMA) (katikati mwenye suti) akiongea na waandishi wa habari jiji Dar es Salaam leo
Mhariri na mwandishi mkongwe wa Habari kutoka gazeti la Uhuru, Noor Shija (kushto) akichangia katika semina ya siku 1 kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam
 Mkurugenzi Mkuu wa  Tume ya Usuluhishi na Maamuzi (CMA) (katikati mwenye suti) akiongea na waandishi wa habari jiji Dar es Salaam leo

Baadhi ya wanahabari wakipitia makabrasha katika semina ya siku moja jijini Dar es Salam kuhusu taratibu za kutatua mogogoro ya kila siku na changamoto zake  sehemu za kazi. Semina hiyo imeandaliwa na Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA)  Wizara ya Kazi na Ajira , ambapo CMA imeeleza  tangu kuzinduliwa kwa TUME mwaka 2007 hadi -30 juni,2012 tume imepokea migogoro 43,003 na kati ya hiyo migogoro 31,125 sawa na asilimia 72.3 imeshapatiwa ufumbuzi.(Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO)
Posted by MROKI On Friday, September 07, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo