Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Rufiji, Dk. Seif Rashid (Kulia) akisalimiana na akina mama wa Kijiji cha Mtanza baada ya kumalizika kwa mkutano na wananchi wa eneo hilo wakati wa ziara ya kuwashukuru wananchi kwa kumchagua kuwa mbunge pamoja na kuwaeleza majukumu mengine aliyonayo sasa ya unaibu waziri.
Dk Rashid akihutubia katika mkutano uliofanyika katika Kijiji cha Mtanza jimboni humo juzi |
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Rufiji, Dk. Seif Rashid (wa pili kukushoto) akiwa na baadhi ya viongozi wa Kata ya Mwaseni, akikagua maendeleo ya ujenzi wa chumba cha darasa wa ziara ya kuwashukuru wananchi kwa kumchagua kuwa mbunge pamoja na kuwaeleza majukumu mengine aliyonayo sasa ya Unaibu Waziri.
Bibi Fatuma Mazengo akilia wakati akisimulia namna mtoto wake na mjukuu wake walivyo uwawa kikatili na Askari wa Wanyamapori katika mpaka wa hifadhi ya Selou maeneo ya Mloka, Rufiji. watu hao wanadaiwa kuuwawa wakati walipokwenda kuvua samaki katika ziwa Mzizizmia. |
Wakazi wa Mibuyu saba wakimsikiliza naibu Waziri huyo. |
Mkazi wa Kijiji cha Tanza, Joseph Nyamgumi, akiuliza swali kwa diwani wao, Athuman Mbange (CUF) ambaye wanadai hana tabia ya kutembelea kijiji chao na kujua kero zao zinazowakabili.
0 comments:
Post a Comment