Agosti 25, 2012 ni siku ya kukumbukwa sana na vijana hawa Denis Mgeni na Haika Masue ambapo Denis alimvisha pete ya Uchumba Haika katika Bustani maridhawa za Magerza Ukonga jijini Dar es Salaam KM Garden tukio ambali lilishuhudiwa na wazazi wa pande zote mbili ndugu jamaa na marafiki. Mungu akijalia wawili hawa watafunga ndoa yao takatifu Mjuini Morogoro Desemba 29, 2012.
Wachumba Denis na Haika wakiwa katika pozi
Mshenga wa Denis Ladislous Ngole akikabidhi Mahari kwa kaka wa Haika, Denis Masue, nyumbani kwao Banana Jijini Dar es Salaam.
Denis Mgeni akiwa na rafiki yake Nico Mwangala aliyemsindikiza na kuwakilisha vijana kadhaa kutoka Mzumbe kushuhudia shughuli hiyo.
Marafiki wa Bi Harusi mtarajiwa Haika nao walikuwepo.
Haika (kushoto) akiwa na marafiki zake.
wachumba wakijipatia chakula
Wazazi wa na wageni mbalimbali wakichukua chakula
Mzee Mgeni (kulia) na ndugu yake wakipata chakula
Ma dada wa Denis pamoja na mama yao wakipata chakula, kulia ni mama mdogo.
Kutoka Mzumbe Denis alisindikizwa na timu ndogo na ya uhakika, hapa ni baadhi yao wakifanya mamambo ya kutia maji katika zege (uchumba) walioushuhudiwa ukiwekwa baina ya Denis na Haika.
Majeshi akiagana na shemeji yake
0 comments:
Post a Comment