Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Barazala Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein,(wa tano kushoto) pamja na Viongozi wengine wa Serikali wakiungana na Waislamu katika Swala ya kuwaombea Dua Abiria waliofariki katika Ajali ya Meli Mv Skagit ya Kampuni ya Seagul,iliyozama hivikaribuni ikitokea Dar es Salaam kuelekea Zanzibar,swala hiyo ikiongozwa na Mufti wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi,katika Msikiti wa Mwembeshauri Mjini Zanzibar leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein,(katikati) pamja na Viongozi wengine wa Serikali wakiungana na Waislamu katika Hitma ya kuwaombea Dua Abiria waliofariki katika Ajali ya Meli Mv Skagit ya Kampuni ya Seagul,iliyozama hivikaribuni ikitokea Dar es Salaam kuelekea Zanzibar, katika Msikiti wa Mwembeshauri Mjini Zanzibar leo
Baadhi ya Waislamu waliohudhuria katika Hitma ya kuwaombea Dua Abiria waliofariki katika Ajali ya Meli Mv Skagit ya Kampuni ya Seagul,iliyozama hivikaribuni ikitokea Dar es Salaam kuelekea Zanzibar, katika Msikiti wa Mwembeshauri Mjini Zanzibar leo.
Katika sala na dua hiyo viongozi mbali mbali wa dini, vyama na Serikali walihudhuria akiwemo Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muunganao wa Tanzania Mhe. Dk. Mohammed Kharib Bilal, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Idd, Rais mstaafu wa Zanzibar Mhe. Dk. Amani Abeid Karume.
Viongozi wengine waliohudhuria ni Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Omar Khabh, Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji, Spika wa Baraza la Wawakishi Mhe. Pandu Ameir Kificho, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib Mhe. Abdalla Mwinyi Khamis, Mawaziri, Manaibu Waziri, Wabunge, Wawakilishi, Mashekhe mbali mbali wa Zanzibar na Tanzania Bara pamoja na wananchi na viongozi wengine.
******
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, leo ameungana na viongozi mbali mbali wa Kitaifa katika dua maalum ya hitma pamoja na Sala maalum ya Maiti (Salatul Mayyit al-ghaib), iliyosomwa huko katika msikiti Mushawar, Mwembeshauri mjini Zanzibar.
Sala na dua hiyo ni maalum kwa ajili ya kuwaombea watu waliokufa kutokana na ajali ya kuzama kwa meli ya MV SKAGIT, iliyotokea hivi karibuni wakati meli hiyo ilipokuwa inasafiri kutoka Dar-es-Salaam
kuja Zanzibar na kusababisha vifo na majeruhi kadhaa
Sala na dua hiyo ni maalum kwa ajili ya kuwaombea watu waliokufa kutokana na ajali ya kuzama kwa meli ya MV SKAGIT, iliyotokea hivi karibuni wakati meli hiyo ilipokuwa inasafiri kutoka Dar-es-Salaam
kuja Zanzibar na kusababisha vifo na majeruhi kadhaa
Katika sala na dua hiyo viongozi mbali mbali wa dini, vyama na Serikali walihudhuria akiwemo Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muunganao wa Tanzania Mhe. Dk. Mohammed Kharib Bilal, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Idd, Rais mstaafu wa Zanzibar Mhe. Dk. Amani Abeid Karume.
Viongozi wengine waliohudhuria ni Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Omar Khabh, Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji, Spika wa Baraza la Wawakishi Mhe. Pandu Ameir Kificho, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib Mhe. Abdalla Mwinyi Khamis, Mawaziri, Manaibu Waziri, Wabunge, Wawakilishi, Mashekhe mbali mbali wa Zanzibar na Tanzania Bara pamoja na wananchi na viongozi wengine.
0 comments:
Post a Comment