Mabingwa watetezi wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame) wataanza kutetea ubingwa wao Julai 14 mwaka huu dhidi ya Atletico ya Burundi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Nicholas Musonye ametangaza ratiba ya michuano hiyo leo (Juni 29 mwaka huu) katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Timu 11 zitashiriki katika michuano hiyo itakayoanza Julai 14 hadi 28 mwaka huu ambapo kwa siku zitachezwa mechi mbili (saa 8 mchana na saa 10 jioni) huku Tanzania Bara ikiwakilishwa na Yanga, Simba na Azam. Mechi ya kwanza siku ya ufunguzi (saa 8 mchana) itakuwa kati ya APR ya Rwanda na Wau Salaam ya Sudan Kusini.
Kundi A lina timu za Simba, URA ya Uganda, Vita Club ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) na Ports ya Djibouti. Azam, Mafunzo ya Zanzibar na Tusker ya Kenya ziko kundi B.
Yanga inaunda kundi C lenye timu za APR ya Rwanda, Wau Salaam ya Sudan Kusini na Atletico ya Burundi.
Timu nane zitaingia robo fainali itakayochezwa Julai 23 na 24 mwaka huu. Kundi A na C kila moja litatoa timu tatu kwenda robo fainali wakati B litatoa timu mbili.
El Merreikh ya Sudan, Red Sea ya Eritrea, Coffee ya Ethiopia na Elman ya Somalia hazitashiriki katika mashindano ya mwaka huu ambayo yanafanyika Tanzania Bara kwa mwaka wa tatu mfululizo kutokana na sababu mbalimbali.
Coffee haitashiriki kwa vile ligi ya Ethiopia inaanza Julai 14 mwaka huu wakati El Merreikh wikiend ya Julai 13-15 mwaka huu itakuwa na mechi ya michuano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).
Bingwa wa michuano hiyo atapata dola 30,000, makamu bingwa dola 20,000 na mshindi wa tatu dola 10,000. Michuano hiyo itaoneshwa moja kwa moja (live) na Televisheni ya SuperSport.
KAGAME CUP 2012 FIXTURE
Sat. 14th July 1 APR vs WAU SALAAM Uwanja wa Taifa 2pm
2 YANGA vs ATLETICO Uwanja wa Taifa 4pm
Sun. 15th July 3 AZAM vs MAFUNZO Chamazi 4p
Mon. 16th July 4 VITA CLUB vs PORTS Uwanja wa Taifa 2pm
5 SIMBA vs URA Uwanja wa Taifa 4pm
Tue. 17th July 6 ATLETICO vs APR Uwanja wa Taifa 2pm
7 WAU SALAAM vs YANGA Uwanja wa Taifa 4pm
Wed. 18th July 8 VITA CLUB vs URA Uwanja wa Taifa 2pm
9 PORTS vs SIMBA Uwanja wa Taifa 4pm
Thu. 19th July 10 ATLETICO vs WAU SALAAM Uwanja wa Taifa 2pm
11 MAFUNZO vs TUSKER Uwanja wa Taifa 4pm
Fri. 20th July 12 PORTS vs URA Uwanja wa Taifa 2pm
13 YANGA vs APR Uwanja wa Taifa 4pm
Sat. 21st July 14 AZAM vs TUSKER Uwanja wa Taifa 2pm
15 SIMBA vs VITA CLUB Uwanja wa Taifa 4pm
Sun. 22nd July REST DAY
QUARTER FINALS
Mon. 23rd July 16 B2 vs C2
17 A1 vs C3
Tue. 24th July 18 C1 vs A2
19 B1 vs A3
Wed. 25th July REST D
SEMI FINALS
Thu. 26th July 20 Winner 16 vs Winner 17
Thu. 26th July 21 Winner 18 vs Winner 19
Fri. 27th July REST DAY
FINALS AND 3rd PLACE PLAY OFFS
Sat. 28th July 22 Loser 20 vs Loser 21
23 Winner 20 vs Winner 21
0 comments:
Post a Comment