Nafasi Ya Matangazo

June 29, 2012

 It’s Ride & Drive time……Kinamama nao wamo.
 Na.Mwandishi wetu
Kampuni maarufu ya kuuza na kusambaza magari nchini Tanzaniaya CFAO Motors kwa mara nyingine imewapa fursa wateja wake kuyajaribu kwa kuyaendeshamagari wanayoyauza na gari mpya aina ya Volks Wagon katika viwanja vya maeneoya Coco beach.

Wateja hao kutoka kampuni mbalimbali wamepata nafasi yakupakia na pia kuyaendesha magari mapya yanayoingizwa hapa nchini na kampunihiyo ili kujua upya na uimara wa magari hayo hivyo kuweza kuchagua magari boraya kununua.

Akizungumza Meneja Masoko wa CFAO Motors Tharaia Ahmedamesema kampuni hiyo imechagua viwanja hivyo kwa kuwa vina sehemu zenye mawe,miinuko na barabara korofi ili wateja wao waweze kuthibitisha uimara wa magariyanayouzwa na kampuni hiyo.

Naye Mkurugenzi mpya wa kampuni mpya ya Alliance Motors Bw.Alfred Minja amesema kampuni yake ambayo ni moja ya makampuni ya CFAO MotorsGroup imeingiza magari mapya aina ya Volks Wagon yakiwemo ‘Amarok’ ikiwa nikatika kuwapatia watanzania nafasi ya kuchagua gari bora wanalolipenda kwagharama nafuu.
 
Nao baadhi ya wateja waliopata nafasi yak u-‘Ride and Drive’wamesifia ubora na upya wa magari hayo na kuhimiza watanzania na kampuni mbalimbli kununua gari hizo.

Dereva wa siku nyingi na mwanajeshi wa zamani Bw. IssaSwalehe amesema kuanzia gari kubwa aina ya ‘Benzi Zitros’ ni nzuri hasa katikasehemu sizizopitika kirahisi na gia zake zinaingia kirahisi kama unavyoendeshagari ndogo.

Kampuni ya CFAO Motors ambayo kwa sasa imefungua kampuni yaAlliance Motors itakayokuwa chini ya Bw. Alfred Minja na kuuza aina tofauti zamagari ya ‘Volkswagon’, Nissan, Benzi na mengineyo hufanya tukio kama hilo lakutoa fursa wa wateja wake ku-‘feel’ ubora wa magari hayo mara tatu kwa mwaka.
 Huu ndio msafara wa magari tofauti ya kampuni ya CFAO MotorsGroup yakiendeshwa na wateja kutoka kampuni tofauti wakati wa Ride & Driveyakiwemo Nissan, Benz, VW ‘AMAROK’ na Suzuki yakichanja mbuga kwenye mabonde namilima kujaribu ubora wake.
 Wateja wa Kampuni ya CFA0 Motors wakibadilishana mawazokuhusiana na ubora wa magari hayo.
 Mkurugenzi mpya wa kampuni mpya ya Alliance Motors Bw. Alfred Minja akipozi na gari yake aina Volks Wagon ‘AMAROK’.
 Meneja Masoko mpya wa CFAO Motors Tharaia Ahmed akiteta na mmoja wa wageni waalikwa.
 Mkurugenzi Mkuu wa CFAO Motors Uganda  Bw. Eric Ruiz akibadilishana mawazo na Meneja Masoko Mpya wa CFAO Motors Tharaia Ahmed.
Posted by MROKI On Friday, June 29, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo