Natumia
siku hii ya Mei 3, kuomboleza: Media ni kama kikosi cha uokoaji.
Inapotokea gari la zimamoto likawaka moto, inapotokea buldoza
linalopaswa kuopoa magari yaliyozama linazama, ujue hali ni MBAYA na ya
HATARI zaidi. Nakumbuka siku ya mafuriko Dar es Salaam, kulikua na picha
mbili zinazonipa tafakuri nzito!
Moja ni ile ya gari la zimamoto na
uokoaji kutumbukia katika maji na ile ya katapila lililofika
Mbezi Beach kuopoa magari lilipozama.
Nikatafakari na sasa naona kama
sisi waandishi wa habari wa Tanzania tumezama katika Taifa la watu
waliokata tamaa wanaohitaji kuokolewa, nani atawaokoa? Naomboleza
nikitoa wito kwa waandishi wa habari kuanzisha mapambano ya kujikomboa
kwanza wenyewe ili tuweze kuikomboa nchi.
0 comments:
Post a Comment