Baadhi
ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kata ya Komnyang'anyo wakitembea
barabarani kuelekea kwenye makazi yao vijiji mbalimbali vinavyoizunguka
shule hiyo.
Makamu
Mkuu Shule ya Sekondari Kivesa, Faustine Mrosso, shule hiyo iliyopo
Kata ya Chanika inahudumia vijiji vya Kwediyamba, Kwedizando na
Kwekambara maeneo ambayo ni mbali na shule hiyo.
Na Joachim Mushi, Handeni
WANANCHI
wilayani Handeni wameilalamikia mazingira magumu kimiundombinu ya shule
za sekondari za kata katika wilaya hilo na kudai ndiyo chanzo cha
kuongezeka kwa mimba kwa wanafunzi na kukatisha masomo.
Kauli
hiyo imetolewa kwa nyakati tofauti katika mahojiano ya baadhi ya wakazi
wa Handeni na mwandishi wa habari hizi ndani ya uchunguzi uliofanywa
hivi karibuni maeneo anuai ya wilaya hiyo kwa ushirikiano na Chama cha
Wanahabari Wanawake (TAMWA).
Abdulah
Mwamponda Mkazi wa Kijiji cha Msasa, wilayani Handeni alisema shule
nyingi za kata zimejengwa mbali na makazi ya wanafunzi jambo ambalo
linawapa mzigo wazazi na wanafunzi kujitafutia usafiri wa kwenda na
kurudi shuleni.
Alisema
katika kijiji hicho wapo wanafunzi ambao hutembea umbali wa kilometa 12
na hata 20 kila siku kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa kwenda na kurudi
shuleni, umbali ambao umekuwa na vishawishi vingi hasa kwa wanafunzi wa
kike kiusafiri.
Alisema
usafiri katika vijiji hivyo ni wa baiskeli na pikipiki (bodaboda) ambao
wazazi wengi wanashindwa kugharamia hivyo watoto kutembea kwa umbali
huo, huku wakati mwingine wakishawishika kupewa msaada wa lifti na
madereva wa bodaboda ambao baadaye huanza kushirikiana nao kimapenzi.
Mzazi
Fatuma Shaban kutoka Kijiji cha Komnyang’anyo alisema wanafunzi wengi
huondoka nyumbani kwao saa 10 za asubuhi na kurudi usiku kutokana na
umbali huo huku wengine wakishinda shuleni bila chochote kutokana na
uduni wa maisha ya kaya nyingi eneo hilo.
Mwalimu
Mkuu wa Shule ya Sekondari Kilimani, Rajab Nyange alisema katika shule
hiyo iliyopo Kata ya Vibaoni nje kidogo ya Mji wa Handeni wapo wanafunzi
wanaotoka vijiji vya mbali takribani kilimeta sita hadi 10 kutoka
nyumbani kwao, ambao hutembea kilomita 20 kila siku yaani kwenda na
kurudi shuleni jambo ambalo linaibua vishawishi kwa wanafunzi.
“Mzazi
anashindwa hata kumpa mtoto wake sh. 100 au 200 kila siku ya shule kwa
ajili ya kula chochote awapo shuleni, je ataweza kumlipia mtoto huyo
gharama za usafiri ambazo ni za juu zaidi kutokana na umbali kutoka
kijiji kimoja hadi kingine,” alihoji Nyange.
Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Hassan Mwachibuzi anasema Ofisi
yake haina taarifa za ubakaji wa moja kwa moja japokuwa anakiri kuwepo
kwa vitendo vya utoro kwa wanafunzi wote kwa sababu mbalimbali. Anasema
pamoja na hayo utoro waweza kuingiliana na ukatishwaji masomo kwa mimba.
Kiongozi
huyu anakiri suala la umbali wa shule huchangia vishawishi kadhaa vya
wanafunzi hasa wa kike kukumbwa na vikwazo kadhaa katika masomo yao.
Hata hivyo anabainisha kuwa uongozi unajitahidi kulitatua suala hilo kwa
kuongeza ujenzi wa hosteli kwa wanafunzi katika shule za kata ili
wanafunzi waondokane na vikwazo anuai.
Aliongeza
kuwa tayari wamejenga hosteli katika maeneo ya Kisasa, Kwamsisi,
Misima, na kudai kuwa wanaendelea maeneo mengine kwa kushirikiana na
wananchi na wahisani huku lengo ni kuhakikisha kila kata inakuwa na
hosteli zake kwa ajili ya wanafunzi wanaotoka maeneo ya mbali na shule.
0 comments:
Post a Comment