wananchi wakiwa wanasaidiana na askari wa zima moto kuzima moto huo
wakati mungine iliwabidi watumie nguvu kubwa
wananchi wakishuhudia zima moto wakizima wakifanya kazi hiyo
mdada akilinda vitu ambavyo amebahatika kuvitoa katika duka alilokuwa akifanyia kazi
Maduka 10 yenye thamani ya zaidi ya
million 100 yameteketea kwa moto katika mji mdogo wa Ngaramtoni wilayaya
Arusha vijijini ambapo chanzo halisi ni hitilafu ya Umeme.
Akiongea na Libeneke la kaskazini katika
eneo la Ngaramtoni mmiliki wa maduka hayo Benjamini Mbayi alisema
kuwa moto huo ulianza majaiara ya saa saba za mchana ambapo ulianza
katika duka moj.
Alisema kuwa wakati moto huo unaanza
alilazimika kuingia kwenye chumba hicho na kuzima umeme katika
kiunganisha cha umeme (SOCKET) lakini bado haikusaidia kabisa na moto
huo uliendelea kutapakaa katikia vyumba bvingine vya biashara.
“Baada ya kuona moshi ukiwa unatapakaa
kwenye paa ambapo kwa kweli nilishindwa kuokoa kitu chochote ila
nilifanya jitiada za kuhakikisha kuwa tunaomba msaada hasa kwa kikosi
cha zima moto jambo ambalo lilifanikiwa ndani ya dakika 30”alisema
Mbayi.
Pia aliongeza kuwa mara baada ya hapo
kikosi hicho kilifanikiwa kuzima moto lakini vitu venye thamani ya
Milioni 100 vilikuwa vimeshateketea kwa Moto lakini kutokana na zoezi
hilo la uokoaji hapakuwa na madhara yoyote yale ya kuunguwa kwa
binadamu
Diwani wa kata ya Olmotony David Kinisi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo alisema kuwa kutokea kwa matukio hayo ya mara kwa mara ya moto katika mji mdogo wa Ngaramtoni kunatokana na ubovu wa mundombinu hasa ya maeneo ya biashara hali ambayo kila mara inasababisha matatizo makubwa sana.
Kinisi alifafanua kuwa tukio la Moto
katika mji huo wa Ngaramtoni ni la Pili ambapo mwezi uliopita maduka
tisa nayo yaliteketea kwa moto huku maduka hayo yakiwa na gharama ya
milioni 200 huku moja ya maduka yakiwa ni mali yake
”kama mnavyoona hapa ubovu wa miundo mbinu unachangia kwa kiwango kikubwa sana na kama halmashauri haoitaweza kuliangalia suala hili kwa undani zaidi basi itakuwa ni hatari sana kwani kuuungua kwa maduka haya ni dalili kubwa snaa ya umaskini hasa Ngaramtoni”alisema Kinisi.
Alifafanua kuwa hali hiyo inatakiwa
kuboreshwa sana hasa katika eneo la Umeme kwa kuwa ndio chanzo kikubwa
Sana cha kutokea kwa majanga ya moto kwa kuwa hata maeneo yaliongua ndio
chanzo kikubwa sana cha hasara na umaskini katika mji mdogo wa
Ngaramtoni.
Awali aliwataka wananchi hasa
wafanyabiashara kuhakikisha kuwa wanafanya biashara kwa kuzingatia
utaalamu wa mafundi wa umeme na wala sio kwa kuwatumia mafundi wa
uchochoroni ambao ndio chanzo kikubwa cha majanga ya Moto.
Naye kamanda wa polisi mkoa wa Arusha
Thobias Andengenye alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo alisema
kuwa bado wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo na kujua thamani
halisi ya maduka yaliyoangua katika janga hilo.
Source: http://www.woindeshizza.blogspot.com/
0 comments:
Post a Comment