Washindi wa Moshi ndio hawa Charlz Mushi, Gaspar Fadhil, a.k.a Chagga Boy na Atufigwege Mwailunga.
Washindi
wakiwa pamoja na majaji, kutoka kushoto ni Charlz Mushi, Jaji Joseph
Haule, Mataluma toka THT, Jaji Queen Darleen, Gasper Fadhil, Atufigwege
Mwailunga na Jaji Henry Mdimu, na mbele kabisa ni Jaji Juma Nature
Majaji wakiwa katika mabishano ya nani apite nani abaki
Baada
ya mikoa ya Mwanza na Dodoma kupata wawakilishi katika shindano la
kusaka vipaji vya mikoani, Kili Regional Talent Search 2012, mkoa wa
kilimanjaro nao jana ulipata wawakilishi watakaoungana na washindi wa
tunzo za muziki za msimu huu, katika tamasha la washindi litakalofanyika
katika viwanja vya Chuo cha Ushirika tarehe 12 ya mwezi huu ambayo ni
Jumamosi ya wiki hii.
Tofauti
na mikoa mingine, Moshi walionekana kuwa na msukumo zaidi katika muziki
wa Hip Hop pamoja na wasichana kuwa na idadi kubwa ya washiriki tofauti
na mikoa mingine ambapo walikuwa hawazidi hata asilimia 5 ya washiriki
wa shindano hilo.
Jumla
ya watu 400 walishiriki katika mchujo wa kwanza, huku majaji wanne
wakiwa katika mchakato huo uliofanyika katika ukumbi wa sinema wa Mr
Price, na hatimaye mpaka kufika mchujo wa pili, ni watu 47 tu walikuwa
wamepatikana kuingia nusu fainali.
Wakiongelea
mchakato huo, kila mtu kwa wakati wake, majaji wa shindano hilo
waliutaja mkoa wa KIlimanjaro, na hasa wilaya ya Moshi kwamba ni sehemu
ambayo walifanya kazi kwa urahisi ukilinganisha na mikoa mingine.
Ila
kama ilivyotegemewa Moshi umekuwa mkoa wa kwanza kutoa mwanamuziki
mwenye kipaji cha Hip Hop jambo ambalo limekuwa faraja sana kwa
mwanamuziki wa kizazi kipya anayeongoza jopo hilo la Majaji, Joseph
Haule a.k.a Professor Jay.
Tofauti
na mikoa mingine, Moshi pia ndio kituo pekee ambacho, licha ya
wasichana wengi kujitokeza kushiriki, hakuna hata msichana mmoja
aliyefanikiwa kufikia hatua ya ushindi, na kupata nafasi ya kushiriki
tamasha la washindi litakalofanyika Jumamosi hii.
Mchakato
wa majaji umewataja Gasper Fadhil a.k.a Chagga Boy, Charl Mushi, na
Atufigwege Mwailunga kuwa wawakilishi wa mkoa wa Moshi.
Washiriki
hawa watapata nafasi ya kila mmoja wao kurekodi wimbo mmoja na kisha
wote kurekodi wimbo wa pamoja, ambazo wataziimba mbele ya mashabiki wa
mkoa wao siku ya Tamasha la washindi.
Mmoja
kati yao atakayefanya vizuri zaidi, atashiriki katika tamasha kubwa la
washindi litakalofanyika mkoani Dar, mapema mwezi ujao.
0 comments:
Post a Comment