Waziri wa Viwanda na Maliasili wa Seychelles, Peter Sinon (kushoto), wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano Mallya (wa pili kulia), mafundi na wawakilishi kutoka Seychelees na Tanzania wakionyesha kipande cha mkongo wa mawasiliano kama ishara ya uzinduzi wa uwekaji wa mkongo wa mawasiliano kutoka jijini Dar es Salaam Tanzania hadi nchini Seychelles katika eneo la Msasani, jijini humo jana. Airtel ni moja ya makampuni yanayosimamia mradi huo.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania, Beatrice Singano Mallya (kushoto) na Meneja Mawasliano wa kampuni hiyo, Jackson Mmbando wakijibu maswali ya wanahabari wakati wa uzinduzi rasmi wa uwekaji wa mkongo wa mawasiliano kutoka jijini Dar es Salaam Tanzania hadi nchini Seychelles katika eneo la Msasani, jijini humo jana. Airtel ni moja ya makampuni yanayosimamia mradi huo.
Mafundi wakiwa kazini wakati wa uzinduzi wa mradi wa uwekaji wa mkongo wa mawasiliano kutoka jijini Dar es Salaam hadi nchini Seychelles jijini humo jana. Airtel ni moja ya makampuni yanayosimamia utekelezaji wake.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania, Beatrice Singano Mallya ( wa nne kushoto) akisaidia kazi ya uwekaji wa mkongo wa mawasiliano kutoka jijini Dar es Salaam Tanzania hadi nchini Seychelles katika eneo la Msasani, jijini humo jana katika hafla ya uzinduzi rasmi wa uwekaji huo ambao Airtel ni moja ya makampuni yanayosimamia utekelezaji wake. Wengine ni mafundi na wawakilishi wa makampuni yanayosimamia mradi huo.
******
Waziri
wa Maliasili na Viwanda wa Shelisheli Bw. Peter Sinon amesema nchi yake
itanufaika na upatikanaji wa mawasiliano ya mkongo wa taifa kutoka
Tanzania kwa ajili ya kuharakisha maendeleo ya taifa hilo.
Mkongo
wa taifa wa mawasiliano uliozinduliwa miaka 2 iliyopita na Rais Jakaya
Kikwete umeweza kuzinufaisha nchi jirani kama Kenya, Uganda,
Rwanda,Burundi na sasa Shelisheli.
Akiongea
katika fukwe za bahari ya hindi jijini Dar es Salaam eneo la msasani
ambako uwekaji wa mlongo huo ndio ulikoanzia mwishoni mwa wiki hii
Waziri Sinon amesema kuwa mpango huo ukimalika utaiweza nchi yake kukuza
sekta ya mawasiliano na upatikanaji wa taarifa mbalimbali jambo
litakalo saidia kukuza uchumi wa nchi hiyo.
“Hii
ni nafasi nzuri ya kipekee na ndio maana hata sisi shelisheli tunaipa
kipaumbele ili kukamilisha zoezi hili la uwekaji wa mkongo huu wa
mawasiliano, tunaamini tukimaliza kila kitu itasaidia sana kukuza pato
la nchi kulingana na umuhimu wa mawasiliano” alisema Bw Peter Sinon-
Waziri wa Maliasili na Viwanda Shelisheli
Kwa
uapnde wake Katibu Mkuu kiongozi kwenye ofisi ya makamu wa rais wan chi
hiyo anayeshughulikia ICT Bw Benjamin Choppy ameelezea faida za uwepo
wa mkongo huo kuwa ni pamoja na kutoa mawasiliano ya uhakika na bora kwa
nchi hiyo
“Sasa
hii ni dalili ya kutoa bidhaa bora ya mawasiliano kwa kuwa ukamilifu wa
uwekaji mkongo huu tutapata mwasiliano bora zaidi” alimaliza kwa kusema
Katibu Mkuu kiongozi kwenye ofisi ya makamu wa rais wan chi hiyo
anayeshughulikia ICT Bw Benjamin Choppy
Nae
Mkurugenzi Mkuu wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania Bi. Beatrice Singano
Mallya ameelezea upatikanaji wa teknolojia hiyo mpya ya mawasiliano kuwa
ni kati ya vitu ambavyo Airtel inavifanyia kazi kuhakikisha
inaunganisha mataifa mengi ili kutoa mawasiliano yanayotoa nafasi au
fulsa ya kuendeleza nchi hizo kijamii na kiuchumi pia
“tunaamini
ushirikiano wetu na wenzetu wa shelisheli ni dhahiri utachangia sana
kuboresha mahusiano yetu kibiashara na pia kutoa nafasi kwa nchi hizi
kujijenga kijamii ma kiuchumu kutokana na faida ya mahusiano haya ya
kulaza mkongo huu wa kuunganisha mawasiliano” alisema Bi Beatrice
Singano Mallya
Aitel
Tanzania na Airtel Shelisheli kwa kushirikiana na SCS zinatekeleza
mpango wa kuweka mkongo wa taifa kwa lengo la kuiwezesha nchi hiyo kuwa
na mawasiliano ya uhakika.
0 comments:
Post a Comment