Zoezi la usafi likiwa linaendelea
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akifyeka maua kuyaweka sawa
katika moja ya bustani katika Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huyo leo
ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Ofisi ya Makamu wa Rais inayozitaka
taasisi za Umma na Serikali kuwa na siku maalum ya usafi wa mazingira
katika maeneo yao. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa imejiwekea utaratibu wa
kufanya usafi kila siku ya alhamisi ya wiki ambapo kila mtumishi
anashiriki katika jukumu hilo. Usafi huo huanza saa mbili hadi saa tatu
asubuhi. Miongoni mwa kazi zinazofanyika ni pamoja kufagia, kufyeka,
uzoaji wa taka ngumu, na usafi wa jumla katika jengo la Ofisi ya Mkuu wa
Mkoa huo.
Kutoka
kushoto ni Afisa Elimu Taalum Mkoa Domician Chose na Kaimu Katibu wa
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Frank Jailos Mateny wakijumuika kwenye usafi huo
leo.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa akipeana neno la mwisho na watumishi wake mara baada ya zoezi hilo la usafi kukamilika.Na www.rukwareview.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment