Nafasi Ya Matangazo

March 09, 2012

 Mwanamke mkazi wa Mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro akiwa sokoni akisubiri wateja wa kuwauzia matango. baada ya kusubiri kwa muda mrefu wanawake hawa wengine waliamua kulala chini. Hii yote ni kutokana na wanawake hawa walivyoamua kujituma na kuamua kufanya biashara.Huyu ameweza kuuza matango wewe unangoja nini.
 Hawa ni wanawake wengine sokoni hapo mjini Moshi katika soko la Mbuyuni wakiuza sukuma wiki. Iwapo wangeamua kulala majumbani na kuwategemea waume zao au ndugu na jamaa haika maisha yao yangekuwa magumu sana. Usiwe tegemezi mwanamke.
 Huyu ni mwanaume anafanya biashara katikati ya wanawake. Wewe mwanamke unangoja nini hapo nyumbani usijitume na kufanya biashara yeyote halali itakayokuingizia kipato chako binafsi na familia na kuachana na utegemezi?. wanawake wanaweza hata bila kuwezeshwa ilimradi tu wawe na afya njema na ubunifu.
Posted by MROKI On Friday, March 09, 2012 1 comment

1 comment:

  1. Kweli Kidevu hujui tabia ya wanaume wa kichagga. Unazani hao wanawake wanapenda kuuza Matango - Kwa taarifa yako wanaume wa kichagga hawajui kutunza familia - wanajua kunywa pombe tuuu -- Hao kina mama wanauza matango ndo wanasomesha watoto, wanawalisha na kuwavisha including hao wanaume wao. Kama huamini fanya uchunguzi!!! By the way mimi ni mchagga.

    ReplyDelete

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo