Nafasi Ya Matangazo

March 19, 2012

Ubunifu ni jambo jema sana miongoni mwa binadamu hasa kama ubunifu huo unamanufaa kwa jamii na mbunifu mwenyewe.  Wengi tumekuwa tukinywa vitu mbalimbali vinavyohifadhiwa katika paketi za plastiki au nailoni lakini mwisho wa siku baada ya kutumia bidhaa hizo tunaishia kutupa na hatimaye kuchafua mazingira tunayoishi.

FK Blog ipo mkoani Iringa, na katika pita pita zake katika mtaa moja na mwingine ilikutana na Grosery hii ya kuuza vinywaji vya aina mbalimbali na kukuta wao pazia lao ni Viroba kama jina la ofisi hiyo. Sijui ni kwanini wameipa jina hilo labda ni kutokana na mauzo mazuri ya kinywaji hicho.

Jamaa wametumia ipasavyo viroba vya Konyagi katika kutengeneza pazia zuri kama ulionavyo pichani, hakika viroba hivi vyote vingekuwa vimetupwa mtaani ni uchafu wa hali ya juu lakini wahusika hapa wamehifadhi mazingira katika hali ya juu. Konyagi mnaweza mpongeza huyu kwa kulinda mazingira mteja huyu na kutoa changamoto kwa wauzaji wengine wa bidhaa hii.
Posted by MROKI On Monday, March 19, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo