Hii ni nguzo ya tatu nayo ipo katikati ya barabara hivyo magari yanapata shida kupita
Hii ndio nguzo iliyowekwa katikati ya barabara mita 100 baada ya nguzo ya kwanza niliyoonesha
Nguzo ambayo imefuata mpaka wa barabara na ipo sahihi
Kwako Meneja wa Tanesco Kisarawe
Jamani mwaka jana mwezi wa kumi na moja nilitoa pongezi kwa viongozi wa Tanesco kisarawe kwa kufanya juhudi ya kuweka nguzo za umeme maeneo ya Pugu kinyamwezi na viunga vyake.
Lakini shughuli hiyo imeishia kwa kuweka nguzo tu na kuziacha kama zilivyo. na mwaka huu mwezi wa pili wamerudi na kuanza kubadilisha nguzo na kuziweka barabarani kwa shinikizo la wenye pesa ili maeneo yao yawe makubwa wakati mawe ya mipaka ya barabara yanajulikana.
Angalia nguzo ya kwanza ilipo , ya pili na ya tatu utajionea mwenyewe. yaani hata mtoto wa chekecheaanauliza mbona nguzo ipo barabarani. pamoja na hayo bado suala la umeme ni kitendawili kwa wakati hawa wa kinyamwezi na viwege. Naomba wahusika wawe makini wasipende kurubuniwa na bahasha au kusikiliza maneno ya viongozi uchwara.Naomba mnipe mawazo itabidi na sisi tufungue kesi kama Nyaronyo ichere anavyowaburuza kwenye mita za luku ambazo walichukua two years.
Regards
XAVERY LANGA KAPECHA NJOVU
0783 662681
MKAZI WA PUGU KINYAMWEZI DAR ES SALAAM







0 comments:
Post a Comment