Mablogger kutoka kushoto ni John Bukuku wa FULL SHANGWE BLOG, Ahmad Michuzi wa JIACHIE BLOG, Joseph Mwaisango kutoka MBEYA YETU BLOG na Mroki Mroki wa FATHER KIDEVU BLOG wakiwa katika picha ya pamoja jijini Mbeya leo hii asubuhi baada ya siku moja jijini milika.
Mablogger hao wapo mkoani Iringa kuripoti matukio mbalimbali katika Maadhimisho ya Wiki ya Maji Kitaifa inayotaraji kufikia kilMachi 22,2012 mjini humo.
Gari la wanalibeneke Hao Likiwa linaondoka kutoka Mbeya kuelekea Iringa Muda huu, Mbeya yetu Blog pamoja na wadau wote Tunawatakia Safari Njema
Wanalibeneke watatu ambao wanajulikana kama Mapacha watatu, Michuzi Jr, Mroki Mroki na John Bukuku leo mapema wamekutana live na Mbeya yetu Blog kwa muda mchache uliopita.
Katika mazungumzo yao mafupi wanalibeneke hao wakongwe nchini Tanzania wameipongeza Mbeya yetu Blog kwa Jitihada ambazo wameendelea kuzifanya za kupashana habari na kusisitiza ya kuwa tuendeleena kasi hiyo hiyo na kuleta habari za uhakika.
Timu nzima ya Libeneke la Mbeya yetu Blog tunapenda kuchukua Fursa hii kuwashukuru sana kwa ujio wenu na kuchukua japo Muda kidogo kuonana nasi. Tunawatakia kila laheri na mafanikio mema. Pia safari njema







0 comments:
Post a Comment