IKIWA imekatika miezi tu tangu Mwimbaji nguli wa Muziki wa dansi Chaz Baba kuhamia bendi ya Mashujaa Musica akitokea Twanga Peteta, inaripotiwa kuwa Mnenguaji mahiri wa kundi hilo la Twanga LILIAN INTERNET na mwanamuziki mwenzake ALY AKIDA wamehamia Mashujaa Musica.
Akizungungumza na blogu hii Meneja wa Mashujaa Musica Maxi Luhanga amesema wanamuziki hao watatambulishwa rasmi Jumatano hii katika ukumbu wa Nyumbani Lounge.
Amesa katika utambulisho huo kundi zima la Mashujaa litasindikizwa na kundio machachari la Machozi Band.
“Hivi tunavyo zungumza tayari wanamuziki hao Internet na Akida wamesha saini mkataba wa Mashujaa Musica na ni wanamuziki wetu na utambulisho ndo huo Jumatano,” amesema Luhanga.
Aidha Luhanga amesema Bendi hiyo inayo zidi kushika kasi na kujizolea mashabiki lukuki hapa nchini imesha kamilisha albam yake ya pili na inataraji kuzinduliwa mapema mwezi mei mwaka huu.
Luhanga amesema albam hiyo yenye nyimbo nane inakwenda kwa jina la TIKISIKA na nyimbo hizo ni pamoja na Umeninyima, ambao wameimba na Nguli wa Musiki wa dansi Papa Wemba.
Nyimbo nyingine ni Ungenieleza, kwa Mkweo, Penzi la Mvutano, Uchungu wa Moyo, Tikisika, hukumu ya Mnafiki wimbo ambao unawania tuzo ya Kili Muzic Award 2012 na unaweza kupiga kura yako kwa kutuma ujumbe mfupi wa “KILI G2 kwenda 15747” wimbo wa mwisho katika albam hiyo ni Nipe Joto.






Ebwana hao Mashujaa wamekuwa mashujaa kweli kweli kumuibia wanamuziki Asaha Baraka.
ReplyDelete