Nafasi Ya Matangazo

March 03, 2012

Blog hii inaungana na wadau wote popote pale Duniani kuwatakia Wanawake Siku yao njema. Mungu awatangulie katika mema yote wanayoyatenda katika jamii. Mwanamke ndio nguzo ya familia katika malezi na binafsi nimekuwa nikiamini hivyo na bado naamini hivyo lakini kadri siku na miaka inavyokwenda wanawake wa siku hizi wamesahau jukumu hilo na matokeo yake wamekuwa ndio waharibufu wakubwa wa maadili katika familia na jamii. 

Wanawake wamekuwa wakivaa mavazi ambayo hayawasitiri kimaumbile na hayo yanafanyika mbele ya wanafamilia na jamii pasi kuwa na woga kwa kigezo cha mitindo. Hivyo wanawake tunawasihi sana mmbadilike na mvae viatu ambavyo bibi zetu hata baadhi ya mama zetu wamekuwa wakivivaa. 
Mungu awabariki wanawake na Mungu aibariki Tanzania.
Posted by MROKI On Saturday, March 03, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo