Blogu ya Father Kidevu leo imesafiri kutoka Mkoani Iringa kuelekea jijini Mbeya. Njiani Blogu hii mbali na kushuhudia manzari nzuri za mikoa hii ya Nyanda za Juu ya Iringa na Mbeya ambayo imetawaliwa na uoto wa asili lakini pia kulikuwa na matukio kadha ya ajali barabarani.
Matukio haya yalikuwa si mengi sana na hakuna tukio ambalo FK Blog ilikuta mtu kapoteza maisha isipokuwa ni uharibifu wa mali na majeruhi.
Pichani ni baadhi ya magari ambayo yalipata ajali kutokana na sababu mbali mbvali ikiwapo za hitilafu za magari hayo ambazo zilichangia ajali hizo.
Madereva wa magari wanashauriwa kuyakagua magari yao kikamilifu na kuyafanyia matengenezo stahiki kabla ya kuanza safari.
Mzee wa Full Shangwe alikuwepo katika msafara huu na hapa akiwajibika kwa staili yake.
Polisi wakikagua ajali hizo
Huyu aliungua kabisa na lilikuwa ni lori la mafuta.










0 comments:
Post a Comment