Nafasi Ya Matangazo

February 25, 2012

Wakazi wa mji wa Moshi na vitongoji vyake jana walianza kujiandikisha kwaajili ya kushiriki mbio mbalimbali za Kilimanjaro Marathon 2012 ambazo pia zinatimiza miaka kumi sasa.

Pichani ni moja ya wakazi hao na wengine kutoka maeneo mbalimbali ya nchi na dunia wakijiandikisha kwaaji ya kukimbia mbio hizo za Kilometa 42 na 21.
 GAPCO Tanzania wao wapo na banda lao na mwaka huu wamedhamini mbio maalum za walemavu za Full Marathon 42km na Nusu Marathon 21km.
Kampuni ya simu za kiganjani ya Vodacom yenyewe imeendelea na udhamini wa Mbio za starehe na kujifurahisha “Fun Run” na hapa ni watu wakijiandikisha kwa wingi kushiriki mbio hizo. Mashindayo ya Kilimanjaro Marathon 2012 yatafanyika kesho Februari 26, 2012 mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro.
Posted by MROKI On Saturday, February 25, 2012 1 comment

1 comment:

  1. CHONDE CHONDE WASIBEBWE NA BODABODA MAANA MWAKA JANA WAS AIBU TUPU... TULIOKIMBIA TUKAKOSA T-SHIRTS KISA WALIOISHIA NJIANI WAKAKODI TAXI KUWAHI ZAWADI ZA VODACOM. KARIBU MOTOWN

    ReplyDelete

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo