Nafasi Ya Matangazo

February 26, 2012

Mashindano ya Kilimanjario Marathon 2012 yamemalizika hivi punde katika mji wa Moshi ambapo wakimbiaji kutoka nchini Kenya wametia fora katika mashindano haya yaliotimiza miaka kumi kwa kunyakua medali zote za Dhahabu, fedha na shaba huku watanzania wakiambulia moja ya shaba.

Pichani ni kundi la wakimbiaji wa Kenya Kilometa 42 wanawake, wakikimbia kwa pamoja na hatimaye kufanikiwa kushinda mbio hizo.
 Mshindi wa Mbio za Kilometa 42 za Kilimanjaro Marathon mkiambiaji kutoka Kenya akimaliza mbio hizo.
 Wakimbiaji wasio washindani wakikimbia mbio za kililometa 21
 Wakimbiaji wa Mbio za Vodacom Fun Run wakikimbia mbio hizo
 Wadau kutoka Precision Air nao walishiriki katika mbio za Fun Run
 Vodacom Kilimanjaro Marathon Fun Run 2012 ikikaribia kuanza
 Mbio za walemavu za Gapco nazo zimetimua vumbi
 Wafanyakazi wa Precision Air wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukimbia.
 Mgeni rasmi , Waziri wa Habari Utamaduni, Vijana na Michezo, Dk. Emmanuel Nchimbi (kulia) akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama uwanjani.
 Washindi wa mbio za Vodacom Fun Run wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi.
 Madam Ritta akimpongeza Binti yake kwa kumaliza mbio za 21KM salama.
 Timu ya CFAO Motors iliyokimbia katika mashindano ya Kilimanjaro Marathon 21km wakiwa katika picha ya pamoja na vionzi.
 Mwanariadha Mkongwe kuliko wote na maarufu katika mbio hizo babu kutoka Arusha akishangilia kumaliza kilometa 21.
 Mkimbiaji akikimbia katika mbio hizo leo
 Mkuu wa Wilaya ya Arusha akitafakari kabla ya kupokea maji mara baada ya kumaliza kilometa 10 za mwanzo kati ya 21 .
 CFAO Motors aliweka meza ya maji na viburudisho katika eneo la kugeuzia Mweka
 Kukimbia ni kazi kama kazi zingine na mkimbiaji unahitajika kuwa na nguvu na pumzi ya kutosha.
 Wakimbiaji wa CFAO Motors wakiwa tayari kwa mbio.
Mkimbiaji upande wa walemavu akikimbia.
Posted by MROKI On Sunday, February 26, 2012 4 comments

4 comments:

  1. kama Moshi kupendeza imependeza leo nyomi, ila bia zinanyweka sijui kesho maofisini inakuaje

    ReplyDelete
  2. Kama walivyotabiri Tanzania itakua nchi ya NDOMBORO na POMBE. Atakukimbia tunashindwa Uyu Kikwete bwana LOL

    ReplyDelete
  3. Kaka,

    Huyo Mtoto wa Madam Rita vipi hapo?
    Keshaolewa huyo au bado?

    ReplyDelete
  4. si mara ya kwanza haya mashindano
    ondoa shaka. business as usual

    ReplyDelete

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo