Nafasi Ya Matangazo

January 25, 2012

shamba darasa lililopandwa kitaalam lililopo katika kijiji cha Kaoze wilaya ya Sumbawanga.
baadhi ya wanakikundi cha CHEMKA wakiwasikiliza wataalam wa kilimo(hawapo) pichani walipowatembelea kijijini kwao Kaoze wilaya ya Sumbawanga.
Baadhi ya Maafisa Kilimo wa Halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga na wakulima wakikagua shamba darasa katika kijiji cha Kaoze wilaya humo juzi.

NA RAMADHANI JUMA-AFISA HABARI WILAYA YA SUMBAWANGA

VIKUNDI vya wakulima katika Halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga Mkoani Rukwa vimeanza kufaidika na miradi ya kilimo kupitia Mashamba Darasa inayodaiwa kuwaongezea mbinu za kisasa za kilimo bora hali inayotarajiwa kuwaongezea mavuno na kipato ikiwa ni juhudi za kujikwamua kutoka katika lindi la umasikini.

Baadhi ya wanachama wa kikundi cha CHEMKA kilichopo katika kijiji cha Kaoze kilichopo bonde la ziwa Rukwa walisema wamenufaika sana na elimu ya mradi wa shamba darasa uliotekelezwa katika kijiji hicho na kwamba wamekuwa wakipoteza mazao mengi kwa kulima kilimo cha kiasili.

Walisema kuwa, kwa kipindi kirefu wamekuwa wakivuna magunia matatu mpaka matano kwa hekari moja walipokuwa wakilima kilimo cha asili lakini kwa kilimo bora cha kisasa wanategemea kupata magunia 25 mpaka 30 kwa hekari moja hivyo wanategemea kujiongezea kipato na kujikwamua katika umasikini.

Kwa mujibu wa Afisa Kilimo wa wilaya hiyo Shaaban Bahari, Halmashauri hiyo ina jumla ya mashamba Darasa 151 katika vijiji mbalimbali wilayani humo na kwamba hali hiyo inatarajiwa kuwafaidisha wakulima.

“Tunategemea miradu hii itawasaidia wakulima wetu kujiongezea mbinu mbalimbali za kilimo cha kisasa ikiwemo matumizi ya mbolea, kupanda kwa kuzingatia nafasi, pamoja na kutumia mbegu bora” alisema Juma.

Miradi hiyo ya mashamba darasa inatekelezwa na wilaya hiyo katika vijiji na Kata mbalimbali kwa lengo la kuwaongezea ujuzi wakulima wilayani humo, ikiwa ni pamoja na matumizi ya mbolea pamoja na mbinu nyingine za kilimo cha kisasa.
Posted by MROKI On Wednesday, January 25, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo