Timu ya Soka ya Yanga ya jijini Dar es Salaam leo jioni imechapwa goli mbili kwa nunge na timu ya Azam FC nayo ya jijini Dar es Salaam katika mchezo wa kirafiki uliopigwa katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.
Yanga iliambulia kipigo hiko leo katika mchezo mzuri na wakusisimua ambapo goli la kwanza lilifungwa na Azam katika kipindi cha kwanza kwa njia ya mkwaju wa penati kupitia kwa mfungaji Gaudence Mwaikimba kabla ya Mrisho Ngasa kumimina Azam Malt ya mwisho na kufanya matokeo kuwa 2-0.
0 comments:
Post a Comment