Nafasi Ya Matangazo

December 10, 2011

 Baada ya kuona wasambazaji wa Filamu wengio ni mizingua na hujinufaisha wao zaidi ya Msanii hwa jamaa wa MIZENGWE ambao ni manguli wa vichekesho pale ITV wameamua kuingia mtaani wao wenyewe na kufanya umachinga wa kuuza filamu yao.

Wasanii hao kadha mbali na kufanya vyema katika vichekso vya kwenye Luninga pale ITV pia wameunda kundi lao linalojulikana kama KASHA KASH.

Mara kadhaa wamekuwa wakionekana katika mikusanyiko ya watu wakiuza filamu yao hiyo na jana walibahatika kunasa wao wenyewe mbele ya Camera ya FK BLOG na hatimaye kupata taswira hizi wakiwa katika Viwanja vya Julius Nyerere almaarufu Sabasaba pale barabara ya Kilwa wakiuza Filamu yao hiyo ya Kash Kash kwa watu waliofika kuangalia maonesho ya miaka 50 ya Uhuru.

Hatua hii ya wasanii hawa ni ya kupongezwa maana wasanii wengi wamekuwa wakiibiwa haki zao na matapeli wachache.
 Wakijadiliana na mteja ili wamuuzie DVD yao hiyo.
 Mkwere nae akifanya ushawishi kwa wateja walau wanunue DVD hiyo.
Watu waliwazunguka na kuwashangaa lakini hapo hapo waliuza kazi yao.
Posted by MROKI On Saturday, December 10, 2011 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo