Mkurugenzi Mtendaji wa Msajili wa Makampuni (BRELLA)Bw. Esteriano Mahingila (kulia) akiongoza timu yake ya vijana wa kazi kutoa huduma kwa wateja na wageni mbalimbali waliotembelea banda la Taasisi hiyo jana wakati wa Maonesho ya Miaka 50 ya Uhuru yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere vilivyopo barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Brella wapo katika maonesho hayo kikazi zaidi kwani huduma za usajili wa makampuni, majina ya biashara Hati Miliki (Trade Mark) na nyinginezo kibao zinafanyika hapo hapo kwa spidi ya ajabu. Father Kidevu Blog ni moja ya makampuni yaliyosajiliwa na BRELLA wakati huu wa maonesho hayo.
0 comments:
Post a Comment