Nafasi Ya Matangazo

December 09, 2011


 Mgeni rasmi Waziri Ofisi ya Rais Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mwinyihaji Makame akikabidhi kombe wa Kampteni wa timu ya wabunge Mh. Amos Makalla, katikati ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya bia ya Serengeti Teddy Mapunda.
 Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya bia ya Serengeti Teddy Mapunda kulia akizungumza na wachezaji wa timu ya bunge Mh. William Ngeleja na Mh. Idd Azzan, kushoto ni Ephraim Mafuru Mkurugenzi wa masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti.

 Kikosi cha timu ya Netiboli wanawake cha Bunge kikiwa katika picha ya pamoja na kombe lao.




 Timu za wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania za wanawake na wanaume zikiwa katika picha ya pamoja na vikombe vyao mara baada ya kushinda michezo yao na kuzifunga timu za baraza la Wawakilishi Zanzibar katika mpira wa miguu na netiboli, katika michezo iliyofanyika jana kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam jana. Michezo hiyo ilikuwa ni kuadhimisha miaka 50 ya uhuru wa Tanzania, ambapo katika netiboli timu ya wanawake iliifunga Baraza la Wawakilishi na Timu ya wanaume katika mpira wa miguu iliifunga Baraza la Wawakilishi magoli 4-1 na kuibuka kidedea huku mfungaji bora wa mchezo huo akiwa Mh. Adam Malima. Timu hizo za Wabunge kutoka Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na ili ya Baraza la Wawakilishi kutoka Zanzibar zilidhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti (SBL)

 Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya bia ya Serengeti Teddy Mapunda kushoto akimpongeza golikipa wa timu Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Idd Azzan mara baada ya timu hiyo kuifunga timu ya Baraza la Wawakilishi kutoka Zanzibar.



 Mgeni rasmi Waziri Ofisi ya Rais Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mwinyihaji Makame akimpongeza Mh.Adam Malima mchezaji wa timu ya Bunge baada ya kuipa ushindi wa magoli 3 kati ya 4, ambayo timu hiyo ilishinda jana baada ya kuifunga timu ya Baraza la Wawakilishi.

 Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya bia ya Serengeti Teddy Mapunda akimpongeza Mh Jma Nkamia wa timu ya Bunge baada ya kushinda mchezo wao jana dhidi ya timu ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar.

 Timu ya Baraza la Wawakilishi wanawake wakielekea kupokea medali zao baada ya kuwa washindi wa pili.

 Mchezaji wa timu ya Wabunge Mh. William Ngeleja akikokota mpira kuelekea lango la wapinzani wao timu ya Baraza la Wawakilishi , wakati wa mchezo wa timu hizo uliofanyika jana kwenye uwanja wa Taifa kuadhimisha miaka 50 ya uhuru wa Tanzania

 Ephraim Mafuru Mkurugenzi wa masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti akikabidhi medali kwa timu ya Barzala la Wawakilishi Zanzibar.

 Chezaji wa timu ya Wabunge akimiliki mpira mbele ya mchezaji wa timu ya Baraza la Wawakilishi jana kwenye uwanja wa Taifa wakati timu hizo zilipokutana kwenye uwanja wa taifa Jana kuadhimisha miaka 50 ya uhuru wa Tanzania.

 Kikosi cha Timu ya Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania
 Kikosi cha timu ya Baraza la Wawakilishi.
 wachezaji wakisalimiana kabla ya kuanza kwa mchezo huo.







Mashabiki waliohudhuria katika mchezo huo wakiushuhudia.
Posted by MROKI On Friday, December 09, 2011 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo