Nafasi Ya Matangazo

December 04, 2011

Mwenzetu Richard Mgamba anaandika;
 
Ndugu yetu Alfred Ngotezi, mmoja wa waandishi maarufu na wakongwe, amefariki dakika arobaini zilizopita huko Arusha baada ya kuanguka ghafla akiwa anaelekea maliwatoni.

Kabla ya kuanguka na kufariki, Ngotezi aliomba kupigiwa wimbo mmoja, akacheza kwa furaha na kisha kupeana mikono na waimbaji huku akiwaambia "tutaonana".


Baada ya hapo Ngotezi aliyekuwa afisa uhusiano wa NSSF, alikaa na kuendelea na mazungumzo na bosi wake kabla ya kukutwa na mauti.

 
Alikuwa Arusha kikazi kuhudhuria mkutano wa kimataifa wa mifuko ya hifadhi ya jamii unaoanza Arusha jumatatu ijayo.

Tumepoteza shupavu katika habari na harakati za kimaisha, Bwana alitoa, Bwana ametwaa, jina lake libarikiwe. Amina
Posted by MROKI On Sunday, December 04, 2011 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo