Mwana dada kutoka mjini Morogoro ambaye anakuja kwa kasi katika anga ya muziki wa Kizazi kipya "bongo Fleva" Dayna Nyange ambae ni tunda kutoka Nyumba ya Vipaji Tanzania (THT) anahabarisha umma kuwa kesho Desemba 18,2011 katika ukumbi wa New Maisha Club anataraji kuzindua Video yake mpya na yakipekee inayokwenda kwa jina la "Nivute kwako".
Aidha Dayna mwenye akiongea na mtandao huu wa kijamii hivi punde anasema video hiyo iliyondaliwa na Mwandaaji Adam Juma kutoka Visual Lab ipo katika viwango vya kimataifa na hakika inatisha hivyo mfike na mjionee wenyewe maajabu yalipo katika video hiyo.
Video yakeo hiyo ya tatu amemshirikisha mkali mwingine kutoka THT ana ambaye anavuma zaidi katika manyimbo ya kibongo bongo hasa ya kimahaba Barnaba Boy. tayari Dayna alisha achia mtaani Video nyingine mbili ambazo ni "Mafungu ya Nyanya" na "Fimbo ya Mapenzi".
Dayna Nyange akiwa katika pozi mwanana la picha.
0 comments:
Post a Comment