Marehemu Rahma Swai (21) enzi zauhai wake.
Mazishi ya Miss Mtwara 2011, Rahma Swai yanataraji kufanyika leo katika makaburi ya Kibamba nje kidogo ya jijini Dar es Salaam imefahamika.
Akizungumza kwa njia ya simu Mwandaaji wa shindano la Miss Mtwara 2011, Rajab Mchata amesema kuwauamuzi huo ulifikiwa jana baada ya mama mzazi wa Rahma kuwasili akitokea nchini Malawi.
Mchata amesema mazishi hayo yanataraji kufanyika leo majira ya saa 7 mchana maeneo ya Kibamba.
Rahma alifariki juzi Oktoba 18 katika Hospitali ya Ligula mjini Mtwara na alikuwa akifanya kazi katika kityuo cha Redio cha Safari FM cha mjini humo.
Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake libarikiwe.Eee Mwenyezi Mungu kuwa pamoja na familia ya marehemu katika kipindi hiki cha majonzi Amina.
ReplyDelete