Nafasi Ya Matangazo

September 25, 2011

Wadau Siddi katikati na Keddy wakipata maelezo ya mmoja wa wataalamu wa makumbusho ya Kaole mjini Bagamoyo wakati walipotembelea makumbusho hayo kama watalii wa ndani, kumekuwepo na kampeni kubwa ya Serikali na taasisi zake zinazohusika na Utalii, kuhakikisha watalii wa ndani wanaongezeka, hivyo kuongeza pato la nchi kupitia utalii wa ndani ukiacha watalii kutoka nje. Mtaalamu huyo anasema kwamba Kisima cha kihistoria cha Kaole kilijengwa mwaka 1250 na waarabu wa kabila la Wapesh kutoka Ghuba ya uajemi, kisima hicho hakikauki maji hata ungechota pipa kadhaa wala hakijai na kufurika maji, hata kama mvua ingenyesha kwa kiwango gani, watu mbalimbali wamekuwa wakichota maji hayo na kuyatumia kwa maana ya kupata baraka kutoka katika kisima hicho.
Kulia ni Mkurugenzi wa FULLSHANGWE BLOG na mdau Keddy wakipata maelezo ya Kaburi lenye kibanda katika maeneo ya makaburi yaliyopo katika makumbusho hayo.
Mti huu una umri wa miaka 507 ni mbuyu na upo katika makumbusho hayo ni moja ya vivutio muhimu katika makumbusho ya Kaole. 
Source: Fullshangwe
Posted by MROKI On Sunday, September 25, 2011 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo