Nafasi Ya Matangazo

September 21, 2011

Mh. Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa na Dr. Wilbrod Slaa, Katibu Mkuu wa CHADEMA. kumbukumbu zangu kama sijakosea wakiwa kwenye shughuli moja inayohusu CCBRT.
Mh Dr. Jakaya Kikwete akikumbatiana na Mh. Profesa Ibrahim Lipumba Mwenyekiti wa Chama cha wananchi - CUF Tanzania

Watanzania wenzangu wanasiasa wetu wanapokua wanakuja kutuomba kura, wanakuja na mengi sana kutoka kwenye vinywa vyao, mengine huwamazuri na mengine ni mabaya maana yanakuwa ni ya kutujengea chuki katika jamii kiasi cha kumuona jirani au hata ndugu yako mbaya. Hivyo basi ni vyema yale wanayoyasema tuyachukulie kama vile tunawaona wako pamoja wamekaa meza moja wakiwa wanatueleza hayo ya kwao. Hili litatusaidia sana kuwafanya wao wasiweze kutugombanisha sisi mpaka kutupelekea kutokea yale ambayo hatutaki yatokee.
 
Ona wao wako meza Moja wanacheka na kufurahi au wamekumbatiana lakini sisi huku hata maji hatuombani.

Father Kidevu Blog + KAPINGAZ Blog inakusihi sana Mtanzania kuwa makini na maneno yao; yatafakari kwanza kabla hujachukua hatua.
Posted by MROKI On Wednesday, September 21, 2011 1 comment

1 comment:

  1. WANABLOG FATHER KIDEVU NA KAPINGA AU KWA WOTE TWAWEZA WAITA DOBLE K MMELONGA YA MAANA SANA NA MUONO WENU NI WA MBALI SANA TUNAPENDA SANA TAARIFA ZA NAMNA HII LABDA ZITAJA LINUSURU TAIFA LETU KWA JUMLA WAKE MDAU - RICHIE WA UGHAIBUNI

    ReplyDelete

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo