Mmoja wa wanamuziki wanaounda kundi la Mapacha 3, Jose Mara, akiimba moja ya nyimbo za kundi hilo usiku wa kuamkia Juni 11, 2011 katika Ukumbi wa Kilimani mjini Dodoma. Hata hivyo show hiyo iliyoanza kushika kasi majira ya Saa 5 usiku iliingia dosari na kushindwa kukata kiu ya wapenzi wa burudani mjini Dodoma pale Polisi wawili walipopanda jukwaani na kumtaka Mara aache mara moja kuimba wakidai muda umekwisha.
Wanamuziki wa Mapacha Watatu wakilishambulia jukwaa katika ukumbi wa Kilimani mjini Dodoma usiku wa kuamkia leo.
Polisi walipopanda jukwaani watu walijua wanapanda kumtunza Jose Mara lakini haikuwa hivyo.
Mashabiki walitulkia na kuangalia nini kinaendelea jukwaani pale. Maana alipanda Polisi wakiume aliyevalia sare pamoja na mwanamke aliyevaa track suti. Awali mashabiki walizani yule mama analindwa na Polisi akienda kutuza.
Burudani ilisitishwa hivi....
Mazungumzo yakifanyika baina ya Polisi, mmoja wa waandaaji na waimbaji.
Polisi alikuwa hataki kupigwa picha...lakini kelele z mashabiki zilimpeleka nje haraka. Polisi hao waliofika ukumbini hapo wakiwa katika Landrover (Diffender) wakiwa zaidi ya wanne, waliendeleaa kuzongwa na watu juu ya tabia yao hiyo huku wao wakidai kupata amri ya kuzima bburudani hiyo kutoka kwa RPC wa Dodoma Zolote Steven, kuamuru saa sita burudani hiyo kuwa mwisho.
Mwaka jana wakati wa tamasha la Wanafunzi wa Vyuo vikuu lijulikanalo kama STR8MUZIK INTER-COLLEGE SPEACIAL 2010 DODOMA lililofanyika Novemba 21, 2010 lilivunjika baada ya Polisi waliokuwa katika pikipi kuvamia na kupita katikati ya kundi la watu zaidi ya 5000 na kupiga risasi hewani kuwatawanya.
Picha hii ni katika Onesho hilo la Mjini Dodoma la Novemba 21, 2010 katika ukumbi wa Royal Village, ofisa wa polisi akizungumza na waandaaji kuwa ameagizwa na RPC kuzuma burudani hiyo majira ya saa sita usiku kama tukio la jana.
Hii ni sehemu ya umati wa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Mkoani Dodoma waliokuwa wamefurika na kutawanywa kwa risasi na pikipiki iliyokatiza katikati yao.
0 comments:
Post a Comment